- Ni kituo kikubwa na Cha kipekee kwenye ukanda wa Afrika Mashariki.( East Africa commercial and Logistics centre)
- Asema Mradi una maslahi mapana ya Taifa kwenye nyanja za uchumi, Biashara na utalii.
- Awaondoa hofu Wafanyabiashara nchini wanaohisi mradi utachangia kushuka kwa Biashara Zao.
- Ampongeza Rais Dkt.Samia kwa ziara zake za kuifungua nchi na kuvuta wawekezaji.
- Mradi ulisimama takribani Miaka 10.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla Leo ametembelea Mradi Mkubwa wa ujenzi wa kituo Cha Biashara Afrika Mashariki unaojengwa Halmashauri ya Ubungo ilipokuwa Stendi ya mabasi ya zamani ikihusisha ujenzi wa maduka zaidi ya 2,060 ambapo Mradi unagharimu shilingi bilioni 280.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, RC Makalla amewaondoa hofu Wafanyabiashara nchini waliokuwa na wakihisi kuwa labda ujenzi wa kituo hicho utakwenda kuzorotesha Hali ya Biashara Zao.
Aidha RC Makalla amesema ndoto na mipango ya ujenzi wa kituo ulianza tangu mwaka 2013 pasipo mafanikio yoyote na kumpongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Kwa kufanikisha jambo Hilo.
Pamoja na hayo RC Makalla amesema ujenzi wa kituo hicho una manufaa makubwa kwa nchi katika nyanja za uchumi, Biashara na utalii.
Hata hivyo RC Makalla amesema manufaa mengine ya mradi ni kusaidia Wafanyabiashara kuagiza mizigo China, Unafuu wa Bei ya bidhaa na kuokoa gharama za nauli na malazi kwa Wafanyabiashara waliokuwa wakifuata mizigo China.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa