-Aagiza kufanyika kwa kikao maalum ndani ya siku 7 ambacho kitaongozwa na yeye mwenyewe
- Asema hakuna anayeweza kujadili au kupinga uamuzi wa mahakama
-Asisitiza busara itumike kufikia muafaka wa mgogoro huo wa Ardhi
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Amos Makalla leo ametembelea na kujionea eneo la mgogoro wa Ardhi Kidagaa Mikenge Wilaya ya Kigamboni Jijini Dar es Salaam.
RC Makalla amepata wasaa wa kulitembelea eneo hilo kujionea uwekezaji uliofanyika na Kampuni ya ACB pamoja na maeneo ya watu wanne ambayo yako mita chache kutoka baharini.
Aidha RC Makalla amesikiliza maoni ya wananchi wa eneo hilo ambao wameomba kuwepo kwa barabara kuelekea baharini, ambapo katika historia inasemekana ilikuwepo, uwepo wa barabara hiyo utawezesha kufanya shughuli zao za kila siku za Uvuvi
Hata hivyo yuko mwekezaji wa Hotel ambaye amesema kwa muda wa miaka 2 sasa hajafanya biashara kutokana na kufungwa kwa njia na kumuomba Mkuu wa Mkoa kunusuru biashara yake kwa kuhakikisha uwepo wa barabara katika eneo hilo
Kutokana na mgogoro huo RC Makalla ameagiza ndani ya siku 7 kuanzia leo Novemba 29,2022 mmiliki wa eneo hilo la Mikenge apatikane yeye mwenyewe, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, Wamiliki wa viwanja 4, Mstahiki Meya, Wawakilishi wa wananchi, na yeye mwenyewe watafanya Kikao cha kufikia Suluhu ya mgogoro huo wa Ardhi.
RC Makalla amesema hakuna kiongozi yoyote yule hapa nchini anaweza kupinga maamuzi ya mahakama hivyo amesisitiza umuhimu wa kutumia busara kufikia Suluhu ya mgogoro huo wa Ardhi eneo la Kidagaa- Mikenge Wilaya ya Kigamboni
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa