- Aagiza Watalaam wa jiji Na ofisi yake waandae michoro Na gharama Za barabara ya kuingia Dampo Na kutoka.
- Awaonya Na ameelekeza uchunguzi ufanyike kwa wanaoiba mafuta ya kuendeshea mitambo ya Dampo
- Aagiza Manispaa zote kutenga maeneo ya madampo kupunguza mlundikano wa taka Dampo la pugu.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla leo ametembelea Dampo la Pugu Kinyamwezi na kujionea ubovu wa Miundombinu ya kuingia na kutoka jambo linalosababisha Magari ya taka kushindwa kumwaga taka sehemu zinazostahili.
Kutokana na kadhia hiyo RC Makalla ameelekeza Wataalamu kutoka Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kuandaa michoro na gharama za Ujenzi wa Barabara za kuingia na kutoka.
Aidha RC Makalla ameelekeza kila Halmashauri kutenga eneo kwaajili ya Ujenzi wa dampo kwakuwa Dampo la Pugu limezidiwa Kutokana na ongezeko la watu Jijini humo na kushindwa kuhimili kupokea taka za Mkoa mzima wa Dar es salaam.
Hata hivyo RC Makalla ameonya na kuelekeza Uchunguzi ufanyike kwa Wezi wa Mafuta ya kuendesha mitambo kwenye Dampo la Pugu ambapo ameita kitendo hicho ni hujuma kwa Serikali.
Pamoja na hayo RC Makalla amesema tayari Zimejitokeza Kampuni 3 kutoka China, Italy na Dubai zilizoonyesha dhamira ya kugeuza taka kuwa umeme ambapo tayari amewapeleka Wizara ya Nishati* kwaajili taratibu nyingine.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa