- Aleta wataalam wa kuboresha usalama wa bahari kwa wafanyabiashara wa eneo hilo
- Asema tayari TANROAD walishafika kwa ajiri ya kuboresha barabara ya kuingia na kutoka Cocobeach
- Asisitiza kuboresha zaidi mandhari sehemu ya mbele kwa kuweka "perving" na "Purms"
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Amos Makalla leo Novemba 9, 2021 amezuru eneo la Cocobeach akiwa ameambatana na wataalam kwa lengo la kutekeleza maelekezo ya Rais Mhe Samia Suluhu Hassan alipotembelea Cocobeach - Kinondoni, Dar es Salaam.
Mhe Makalla amesema wataalam hao wameletwa ili kuweka mawe ili kulinda kingo ya bahari ambayo ni kwa ajili ya USALAMA wa bahari na wafanyabiashara wadogo wanaofanya Shughuli zao katika eneo hilo kutokana tabia ya maji kupanda na kushuka.
Aidha Mkuu wa Mkoa amesema wataalam hao pia wataweka "perving" eneo la mbele kwa ajili ya kuzuia vumbi na kupanda "Purms" ili eneo hilo liwe na mvuto.
Sambamba na hilo Mhe Makalla amesema tayari TANROAD walishafika jana kwa ajiri ya kuboresha barabara ya kuingia na kutoka ndani ya Cocobeach na kazi hiyo itafanyika haraka iwezekanavyo.
"Tunaendeleaa kuboresha Cocobeach, ivutie na fukwe hiyo ni kwa ajili ya watu wote, YAJAYO YANAFURAHISHA" Alisema RC Makalla
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa