- Wazalishaji Mifuko mbadala waomba Serikali kuchukuwa hatua.
- NEMC na TBS Watoa tamko la kusimamia Operesheni, Wataka Mikoa ya mipakani kuimarisha Udhibiti.
- RC aagiza kuitishwa kikao Cha Wenyeviti wa Masoko DSM.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla leo August 19 ametangaza Operesheni ya kukamata Mifuko ya plastic iliyokatazwa na kuwataka Wananchi kujiepusha na Matumizi ya Mifuko hiyo.
RC Makalla ametangaza Operesheni hiyo wakati wa kikao kazi Wazalishaji Mifuko mbadala, Kamati ya Ulinzi na usalama na Mamlaka za Udhibiti ikiwemo TBS na NEMC Baada ya kubaini Mifuko iliyokatazwa imeanza kurudi upya
Aidha RC Makalla ameagiza kuitishwa kikao Cha Wenyeviti wa Masoko yote ya Mkoa huo na kutolewa maelekezo ya katazo la uuzaji wa Mifuko iliyokatazwa kwenye Masoko yao.
Pamoja na hayo RC Makalla ameelekeza Mamlaka ya Udhibiti na usimamizi wa Mazingira NEMC kurudi upya kutoa Elimu kwa Wananchi kuhusu Madhara ya Matumizi ya Mifuko hiyo.
Miongoni mwa Madhara ya Matumizi ya Mifuko iliyokatazwa ni Uchafuzi wa Mazingira, Ukwepaji wa Kodi Kutokana na Mifuko Kuuzwa kinyemela pamoja na viwanda vilivyopewa kazi ya kuzalisha Mifuko mbadala.
Kwa upande wao Mamlaka za Udhibiti kupitia Wakurugenzi wa NEMC na TBS wametumia kikao hicho kutoa tamko la kusimamia Operesheni hiyo ambapo wamemuahidi RC Makalla kuwa Operesheni hiyo itafanikiwa.
Nao Wazalishaji wa Mifuko mbadala wamekiri uzalishaji wa Mifuko iliyoruhusiwa kudorora Kutokana na kuzagaa kwa Mifuko iliyokatazwa kwenye Masoko na Maduka jambo linalopelekea viwanda vyao kufa ambapo wameiomba Serikali kusimamia Operesheni hiyo
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa