- Aelekeza Ardhi iliyovamiwa zaidi ya Ekari 6000 za NSSF na DDC zirasimishwe kwa kupima viwanja na Wananchi kununua viwanja hivyo
-Aagiza kila Taasisi inayomiliki eneo Jumatatu Agosti 15,2022 wafike Mabwepande kuhakiki mipaka yao na kuyalinda maeneo hayo
-Asema Uamuzi umezingatia mapendekezo 19 ya kamati ya wataalam aliyoiunda kushughulikia mgogoro wa Ardhi zaidi ya Wananchi 4000 waliofika na kuhakikiwa na kamati
-Wananchi wa Mabwepande wamefurahishwa na kupongeza Uamuzi wa Serikali
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Amos Makalla leo Agosti 10,2022 *ametembelea na kukagua zaidi Ekari 6000 za NSSF na DDC ambazo zimevamiwa na Wananchi Kata ya Mabwepande Kinondoni-Dar es Salaam.
RC Makalla akiongea na umati wa Wananchi katika viwanja vya Kata ya Mabwepande baada ya kukagua eneo lililovamiwa *ametangaza rasmi kumaliza mgogoro wa Ardhi Kata ya Mabwepande kwa kutoa maelezo yafuatayo.
Mosi RC Makalla ameelekeza Ardhi iliyovamiwa na Wananchi zaidi ya Ekari 6000 za NSSF na DDC Kurasimishiwa na kupimwa viwanja na Wananchi wapewe fursa ya Kuzinunua viwanja hivyo kipaumbele kiwe kwa wananchi wa eneo hilo.
Aidha RC Makalla ameagiza kila Taasisi inayomiliki eneo Mabwepande Jumatatu Agosti 15,2022 wafike Kuhakiki mipaka yao na kuanzia hapo maeneo ya lindwe ili yasivamiwe tena.
Vilevile Mhe Makalla amesema Uamuzi alioufanya umezingatia mapendekezo 19 ya kamati ya wataalam aliyoiunda kushughulikia mgogoro wa Ardhi ambapo zaidi ya Wananchi 4000 walifikiwa na kamati na kuhakikiwa na uhakiki huo ulithitisha kuwa eneo hilo limevamiwa na kubaini wamiliki halali.
Hata hivyo kufuatia maamuzi hayo ya Serikali Wananchi wa Mabwepande wamefurahia na Kupongeza Uamuzi huo na kuahidi kushirikiana na Serikali bega kwa bega ili migogoro kama hiyo isitokee tena.
Ifahamike kuwa kumaliza kwa mgogoro wa Ardhi Mapwebande ni moja ya Migogoro mingi ya Ardhi katika Mkoa wa Dar es Salaam iliyomalizwa chini ya Uongozi imara wa RC Makalla toka ateuliwe na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa