- Asema Awamu ya kwanza imekuwa na Mafanikio Makubwa ya kudhibiti biashara Holela, usafi Na uondoshaji takataka.
- Awamu ya pili ni upendezeshaji ikiwemo, upandaji miti, bustani na upakaji rangi nyumba kwenye Smart Road.
- Ataka Kila Halmashauri Kuanza maandalizi ya kampeni ya Usafi mtaa kwa mtaa.
- Aongoza Kikao kazi cha kuweka mikakati ya kuelekea awamu ya pili ya kishindo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam CPA, Amos Makalla leo ametangaza Kuanza kwa awamu ya pili ya kampeni ya SAFISHA PENDEZESHA DAR ES SALAAM baada ya awamu ya kwanza ya kampeni hiyo iliyodumu kwa mwaka Mmoja na miezi 5 kuwa na Mafanikio Makubwa ikiwemo kufanya Jiji Hilo kushika nafasi ya Sita kwa usafi Afrika.
Akizungumza wakati wa kikao kazi Cha tathimini awamu ya kwanza na kuweka mikakati ya awamu ya pili,CPA, Makalla ameelekeza watendaji kuanzia ngazi ya Mkoa, Wilaya, Kata na Mitaa kusimamia ufanyaji Usafi.
Aidha CPA, Makalla amesema miongoni mwa mambo yayopaswa kuwekewa mkazo zaidi ni udhibiti wa ufanyaji biashara holela, usafishaji mazingira, upendezeshaji na upandaji miti kwenye bustani.
Kutokana na Mwamko mkubwa wa usafi uliopo, RC Makalla ameelekeza Kila Halmashauri kushirikiana na wadau ambao wapo tayari kupendezesha Jiji huku akielekeza Taasisi za TANROAD, TARURA na DAWASA kufanya kazi kwa ushirikiano.
Pamoja na hayo CPA, Makalla amesema lengo la kampeni hiyo ni kufanya Dar es salaam izidi kushika nafasi za juu kwa usafi Afrika jambo litakalosaidia kudhibiti pia mlipuko wa magonjwa ya mlipuko ikiwemo Kipindupindu na hata kudhibiti maambukizi ya malaria.
Hata hivyo RC Makalla ameendelea kusisitiza Wananchi kufanya usafi Kila ifikapo jumamos ya mwisho wa Mwezi huku akiwataka wafanyabiashara kufanya biashara kwenye Maeneo waliyopangwa
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa