- Abainisha itakuwa ni sehemu nzuri ya kupumzika na burudani babukubwa "Vibe la kutosha"
- Asema fukwe ya COCO hajapewa mwekezaji bali wameshirikishwa wadau kwa ajili ya kuboresha.
- Asisitiza waliokuwa wanafanya biashara katika eneo hilo hawataondolewa ndio maana waliorodheshwa
- Awahakikishia usalama wa kutosha katika eneo la Coco beach
- Awataka vijana kuweka Mkakati wa usafi katika fukwe hiyo, asema COCO pataitwa " Dar sunset Canival "
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Amos Makalla leo Septemba 29, 2021 amefanya kikao kazi na Makampuni ya Vinywaji Katika fukwe za Coco beach Kinondoni jijini Dar es salaam.
Akiongea na wafanyabiashara hao Mkuu wa Mkoa ametangaza Dar Sunset Canival ndani ya Cocobeach ambapo kutakuwa na burudani babukubwa na itakuwa sehemu nzurii ya watu kupumzika.
Vilevile amesema Serikali inawapenda wafanyabiashara wadogo wadogo hivyo *wasipotoshwe na mtu yeyote kuwa wanafukuzwa, amewahakikishia hakuna atakayefukuzwa* bali wanaboresha eneo hilo liwe na mwonekano mzuri, livutie kwa ajili utalii na watu kupumzika
Mhe Makalla amesema fukwe ya COCO hajapewa mwekezaji isipokuwa wameshirikishwa wadau wa Biashara katika kuboresha fukwe hiyo iwe na mwonekano mzuri hatimaye ivutie Utalii na watu wapate sehemu ya kupumzika.
" Coco beach itakuwa ni ya watu wote wenye vipato vikubwa na vidogo wataweza kutembelea kupumzika na kupata burudani pataitwa Dar Sunset Canival " Alisema Mhe Makalla
Aidha Mkuu wa Mkoa amesema kwa kuwa yeye ndiye mwenyekiti wa Ulinzi na Usalama, amewahakikishia Usalama nyakati zote hakutakuwa na kibaka au mateja katika fukwe hiyo.
Sambamba na hilo Mhe Makalla amesema katika fukwe hiyo Makampuni yafuatayo ndio wadau muhimu katika uboreshaji wa fukwe hiyo Cocacola, Pepsi, Azam Group, TBL, CRDB, na NMB
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa