Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makalla leo tarehe 07 Oktoba, 2021 amefanya Kikao Kazi na Viongozi na Watendaji katika Ukumbi wa Iddi Nyundo uliopo Wilayani Temeke ambapo ametaka Maelekezo Mahususi 11 kutekelezwa na Viongozi na Watendaji ili kuujenga vema Mkoa wa Dar es Salaam
Maelekezo hayo Mahususi ni pamoja na:-
✓ Upangwaji mzuri na Shirikishi wa Wamachinga ambapo Wamachinga hao kwa kushirikiana na Viongozi wa Wilaya zote wameendelea kuyatambua maeneo yao aidha, Wakurugenzi wametakiwa kupeleka huduma zote za Kijamii sambamba na LATRA, Jeshi la POLISI kufikisha Magari katika maeneo hayo
✓Maafisa Maendeleo ya Jamii kuandaa Kongamano kubwa katika Ukumbi wa PTA kuhusu Jukwaa la Kuwawezesha Wanawake kiuchumi katika Mkoa wa Dar es Salaam ambapo wanatakiwa kuandaa *ndani ya wiki ya Pili ya mwezi wa 11
✓Kuhakikisha Asilimia 60 ya Mapato ipelekwe kwenye Miradi ya Maendeleo kwani toka Mhe. Rais Samia aingie madarakani hakuna Mradi uliosimama yote inaendelea hivyo ni muhimu kuzingatia hilo
✓Changamoto katika maeneo ya pembezoni zitatuliwe ambapo Tanesco wapeleke Umeme Dawasa- Maji ,Tanroads na Tarura kuwajengea wananchi Barabara
✓Ukaguzi Miradi ya Maendeleo Mhe. Mkuu wa Mkoa amewataka kuwa wepesi, makini katika kukagua miradi ya maendeleo ambapo aliunda kamati Maalum ya kudumu ya kufuatilia miradi ya Dar es Salaam
✓Kusikiliza na kutatua KERO za Wananchi ambapo amewataka Wakuu wa Wilaya pamoja na Wakuu wa Idara kwenda Kata kwa Kata kusikiliza na kutatua KERO za wananchi na kila mwisho wa mwezi kuandika taarifa
✓Waganga Wakuu wa Wilaya kuhakikisha Hospitali zote zinakuwa na Dirisha la Wazee, uwepo wa Dawa zote muhimu na Wazee wapokelewe na kuhudumiwa vizuri
✓Uhifadhi wa Mito na Mazingira Mhe. Makalla amepinga zoezi la uchimbaji wa michanga na kusisitiza usafi,Usalama wa mito ambapo Muongozo wa kutunza Mazingira ameshausaini na kuutuma
✓Chanjo ya Uviko 19 ambapo Dar es Salaam imefanya vizuri katika hili na kuwataka ambao bado hawajachanjwa wakachanjwe
✓Ulinzi na Usalama ambapo amesema Dar es Salaam ni salama na kutaka kuendelea kudumisha Amani na Utulivu na Kama kuna mhalifu afichuliwe
✓Uendelezaji wa Fukwe ambapo Kuna Fukwe nzuri zinazotakiwa kusafishwa na kuboreshwa hivyo Maafisa Mazingira wote wanatakiwa kwenda COCO BEACH kujifunza
"Viongozi na Watendaji tekelezeni wajibu wenu katika kuwahudumia wananchi, tusikae maofisini, tuwafuate wananchi walipo na kuwahudumia" Alisisitiza RC Makalla
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa