-Asema Wazee wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba katika Wilaya ni watu muhimu, awataka kufanya kazi kwa weledi na Uaminifu
-Abainisha Wakati anasikiliza kero za wananchi katika Majimbo 10 DSM asilimia kubwa ya migogoro ni ya Ardhi
-Aahidi kufanya kikao cha pamoja na wajumbe wa Mabaraza ya Ardhi DSM, awapongeza waliokula kiapo leo Manispaa ya Ubungo na Kigamboni
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Amos Makalla leo Februari, 14, 2021 amewaapisha wajumbe wa Baraza la Ardhi na Nyumba Manispaa ya Ubungo na Kigamboni Ofisini kwake Ilala boma Jijini Dar es Salaam
RC Makalla ametoa wito kwa wajumbe wa Mabaraza katika Wilaya zote za Mkoa wa DSM kuwa Mahakama ya Rufaa pale migogoro ya Ardhi inapotokea, *Chombo hicho muhimu kiaminiwe na wananchi wakiwa na Changamoto yoyote ya Ardhi watambue sehemu sahihi ya kuweza kutatuliwa ni katika Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya husika*
Aidha RC Makalla amesema wakati anasikiliza KERO za wananchi katika Majimbo 10 ya Mkoa wa DSM asilimia kubwa ya migogoro aliyokutana nayo ni ya Ardhi na wengi walikuwa wakisema Mabaraza ya Ardhi hayatendi haki hivyo ni wakati muafaka sasa kufanya kazi kwa weledi na Uaminifu.
"Hadi unateuliwa kuwa mjumbe wa Baraza la Ardhi na Nyumba katika Wilaya inamaana umeaminiwa na rekodi za maisha yako katika Jamii inayokuzunguka ni nzuri hivyo kaitendeeni haki nafasi hiyo" Alisema RC Makalla
Hata hivyo kwa kutambua Umuhimu wa Mabaraza hayo katika utatuzi wa migogoro ya Ardhi DSM RC Makalla ameahidi kufanya kikao cha pamoja na Mabaraza hayo kwa Mstakabali wa kuboresha Utoaji huduma wa Mabaraza hayo.
Vilevile RC Makalla amesema amewaagiza Wakurugenzi wa Manispaa za Mkoa wa DSM kuimarisha Mabaraza hayo ikiwemo kuhakikisha kunakuwa na vitendea Kazi
Kwa Upande wa mwenyekiti wa Baraza la Ardhi Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Ramadan Matumbwa akiongea wakati wa hafla hiyo amesema Uzee ni dawa, dawa hiyo iende ikatibu magonjwa ya migogoro ya Ardhi katika Wilaya.
Ifahamike kuwa kuwepo kwa Wazee au wajumbe wa Mabaraza ya Ardhi ni takwa la kikatiba, wajumbe hao huudumu nafasi hiyi kwa Kipindi cha miaka 3 siku ya leo RC Makalla amewaapisha wajumbe 4 toka Manispaa ya Ubungo na Wajumbe 2 Manispaa ya Kigamboni
Hafla hiyo imehudhuriwa na Katibu Tawala Mkoa wa DSM Ndg Hassan Rugwa, Naibu Kamishna Ardhi Mkoa DSM, Msajili wa Ardhi, Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi na Nyumba Mkoa, na Wataalam wengine toka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa