- Atinga Kiwandani na kuitisha Kikao cha Wabia wa DAR BREW (CHIBUKU) ambao ni Jiji, Manispaa ya Kinondoni, na Manispaa ya Temeke
- Asema dhana ya Serikali kufanya biashara katika uchumi wa Soko imepitwa na wakati Ubia ndiyo njia nzuri
-Wawekezaji wameanza kujitokeza kutaka kuwekeza
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam CPA Amos Makalla leo Februari 13, 2023 ametembelea na kukagua kiwanda cha DAR BREW cha kutengeneza pombe maarufu kwa jina la Chibuku kilichoko Wilaya ya Ubungo Jijini Dar es Salaam.
CPA Makalla akiwa katika kiwanda hicho amepata wasaa wakujionea mitambo na samani mbalimbali zinazo milikiwa na kiwanda hicho ambacho uzalishaji wake umesimama toka mwaka 2018
Aidha CPA Makalla baada ya kukagua mazingira ya kiwanda hicho amesema kiwanda hicho lazima kifufuliwe ambapo ameitisha kikao cha Wabia wa DAR BREW (Chibuku) ambao ni Jiji, Manispaa ya Kinondoni na Manispaa yaTemeke kesho Februari 14, 2023 kukutana kujadili mstakabali wa kufufua kiwanda hicho kwa masilahi mapana ya Umma.
Sambamba na hilo CPA Makalla amesema dhana ya Serikali kufanya biashara katika uchumi wa Soko imepitwa na wakati bali UBIA ndiyo njia nzuri hivyo kila mmoja wetu lazima abadilike ili kuwezesha kukuza ajira na Serikali kujipatia mapato yake.
CPA Makalla amewahakikishia tayari Wawekezaji wameanza kujitokeza kutaka kuwekeza ni wajibu wetu kutokurudi nyuma lazima twende sambamba na maono ya Rais Dkt Samia Suluhu katika kuandaa mazingira rafiki ya uwekezaji
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa