RC Makalla akiongoza wananchi kupanda miti zaidi ya 2000 mapema leo Kata ya Bunju-Kinondoni
-Amesema Rais Dkt Samia na Viongozi wengine Duniani wameelekeza umuhimu wa kutunza MAZINGIRA Na kupanda miti kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya Nchi
-Aishukuru Benki ya NMB kwa ufadhiri wa Kampeni ya Upandaji na Utunzaji miti pamoja na TFS kwa kugawa miche ya miti bure
- Awataka Viongozi wa ngazi zote DSM kuhamasisha Upandaji na Utunzaji wa miti katika maeneo yao
Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam CPA Amos Makalla amewataka kila mwananchi kwenye nyumba yake katika mkoa huo kupanda miti rafiki ili kuunga mkono juhudi za Serikali za kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.
CPA Makalla ameyasema hayo leo katika viwanja vya Shule ya Sekondari Michael Tarimo iliyoko Kata ya Bunju, Manispaa ya Kinondoni *wakati akizindua Kampeni ya upandaji miti kwa Mkoa wa Dar Es Salaam
Aidha CPA Makalla amesema licha ya kuwa zoezi la kupanda miti ni maelekezo ya Ilani ya CCM, Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ametoa maelekezo hayo kwa msisitizo mkubwa yeye binafsi, vilevile hata Viongozi wengine Duniani wameeleza umuhimu wa kuwa na Kampeni ya kupanda miti ili kutunza mazingira ambayo ndio njia nzuri ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.
CPA Amos Makalla ameishukuru Benki ya NMB kwa kufadhiri Kampeni ya kupanda miti na kutenga fedha zaidi ya Bilioni 4 kuhamasisha Upandaji na Utunzaji miti nchini, pia amezitaka taasisi zingine za kifedha kuiga mfano wa NMB, hata hivyo amewapongeza TFS kwa kutekeleza wajibu wao kwa kuwezesha kutoa miche ya miti zaidi ya elfu 28 bure.
Sambamba na hilo CPA Makalla ameagiza Viongozi wa ngazi zote DSM kuhamasisha Upandaji na Utunzaji wa miti katika maeneo yao kwa nguvu zote ambapo amesema ni matarajio yake pesa zitakazotolewa na NMB kwa washindi wa Utunzaji wa Mazingira, washindi wote watoke Dar Es Salaam.
Ifahamike kuwa katika Uzinduzi huo leo April 08, 2023 CPA Makalla ameongoza wananchi kupanda miti mbalimbali ya kivuli, matunda na mbao takribani elfu mbili (2000)
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa