- Ataka Barabara zote kubwa DSM zitunzwe, zisafishwe, bustani nzurii na kupandwe miti
- Awataka Wananchi wote kuwa na utamaduni wa kuchukia uchafu
- Aagiza Wakandarasi wa usafi kuzoa taka kwa wakati
- Apongeza Temeke kwa kukusanyika kufanya usafi wa pamoja, asema DSM imefakiwa sana Kampeni yake ya Safisha pendezesha DSM
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam CPA Amos Makalla mapema leo ameungana na wakazi wa Wilaya ya Temeke kufanya usafi wa pamoja kuanzia Quality Plaza hadi Tazara Barabara kuu ya Kutoka Airport kwenda Posta
CPA Makalla ameelekeza Barabara zote kubwa Katika Mkoa huo *zitunzwe, zisafishwe, zitengenezwe bustani za watu kupumzika zenye maua yanayovutia na kupandwe miti mizuri ikiwa ni muendelezo wa Kampeni ya SAFISHA PENDEZESHA DSM, kazi ya kutengeneza bustani ifanywe na Taasisi au Makampuni ambayo majengo yao yapo pembeni mwa barabara.
Aidha CPA Makalla amewataka wananchi wote wa Mkoa wa Dar es Salaam kuwa na utamaduni wa kuchukia uchafu kila mmoja awe na wazo kuwa Usafi unaanza na yeye.
Vilevile CPA Amos Makalla amepongeza makampuni ya Usafi yanayofanya vizuri katika kuzoa taka kwa wakati hivyo ameagiza wakandarasi wengine waache kufanya kazi kwa mazoea wahakikishe wanazoa taka kwa wakati
Sambamba na hilo CPA Makalla amesema toka kuanza kwa kampeni ya Usafi DSM imefanikiwa kwa kiasi kikubwa rai yake ni kutorudi nyuma tusonge mbele hadi DSM ishike nafasi ya kwanza na mkakati wa Mkoa katika kuopambana na magonjwa ya milipuko ni Usafi
Mwisho CPA Makalla amesema Usafi ni wa watu wote hauna Chama amewapongeza wakazi wa Temeke kwa kujitokeza kwa wingi kufanya usafi wa pamoja siku ya leo
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa