-Aagiza Bodi ya DDC Kuhakiki mali zote na Kuzirejesha
-Alitaka Shirika hilo kuandaa Mpango Mkakati wa Kibiashara " Strategic Business Plan"
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Amos Makalla leo Agosti 9,2022 amekutana na Viongozi wa Shirika la Uchumi na Maendeleo ya Biashara Jiji la Dar es Salaam (DDC) katika Ukumbi mdogo wa mikutano ulioko Anatoglo Mnazimmoja Ilala Jijini Dar es Salaam.
Akiongea na Viongozi hao ameeleza dhamira yake ya kulitaka Shirika hilo kujiendesha Kibiashara ili liweze kupata faida ambayo italiwezesha kutoa Gawio kwa Serikali kama ilivyo kwa mashirika mengine.
Aidha RC Makalla ametoa agizo ili kufikia adhima hiyo kwanza kufanya uhakiki mali zote za shirika na Kuzirejesha chini ya DDC na ujereshaji wa mali hizo kwa Upande wake kama kiongozi wa Mkoa kesho Agosti 10, 2022 atembelea kakagua na kurejesha eneo la Hekari zaidi ya 1931Mapwebande- Kinondoni* ambazo ni mali ya shirika hilo.
"Mtazamo wangu nikiwa Mkuu wa Mkoa huu Shirika lijiendeshe Kibiashara zaidi na Safari ndio hii imeanza" Alisema RC Makalla
Sambamba na hilo RC Makalla amelitaka shirika la DDC kuwa na mpango mkakati wa Kibiashara ambao utawawezesha kila eneo wanalo miliki kujua watalifanyia nini hata kama kuna uhaba wa rasilimali fedha wanaouwezo wa kutafuta wawekezaji wakawekeza na shirika likapata faida.
Shirika la Uchumi na Maendeleo ya Biashara Jiji la Dar es Salaam (DDC) ni miongoni mwa mashirika Kongwe Nchini ambalo kwa sasa limekuwa halifanyi vizuri hivyo Maono ya RC Makalla ni mwarobaini wa Shirika hilo kuwa na manufaa kwa wananchi wa DSM na Taifa kwa Ujumla
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa