- Ampongeza *Rais Dkt, Samia Suluhu Hassan kufanikisha mradi huo uliogharimu zaidi ya Shilingi bilioni 90.*
- Awapongeza *DAWASA kwa Kasi ya kuwaunganishia Wananchi Maji.*
- Wananchi *wanapatiwa Maji ya mkopo.*
- Akemea *urasimu kwenye kuwaunganishia Wananchi Maji.*
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam *CPA, Amos Makalla* leo amefanya ziara ya kukagua usambazaji wa huduma ya Maji *Mtaa kwa Mtaa, Nyumba kwa Nyumba* kwa Wananchi Kata ya *Mivumoni* Wilaya ya Kinondoni baada ya kukamilika kwa mradi mkubwa wa Maji uliogharimu zaidi ya *Shilingi bilioni 90.*
Akizungumzia wakati wa Ziara hiyo iliyokwenda sambamba na*kukabidhi Vifaa* kwa Wananchi, *CPA Makalla* amewapongeza *DAWASA* kwa Kasi kubwa ya kuwaunganishia Wananchi Maji.
Aidha *CPA, Makalla* amewaelekeza *DAWASA* kuhakikisha unganishaji huo unaenda sambamba na *kuhakikisha Maji yanatoka* huku akisisitiza utoaji wa *Control number* kwa wakati.
Pamoja na hayo *CPA, Makalla* amekemea tabia ya *urasimu* kwenye kuwaunganishia Wananchi Maji ikiwemo kutoa huduma kwa *upendeleo au kujuana* na kusisitiza kuwa *Mwananchi anaefanya malipo apatiwe vifaa kwa wakati.*
Kuhusu Suala la unganishaji Maji kwa Mkopo, *CPA Makalla* amewaelekeza *DAWASA* kusimamia ahadi hiyo na kuwataka Wananchi kuwa wepesi kwenye *kulipa*.
Kwa Upande wake Kaimu mtendaji mkuu wa DAWASA *Eng. Shaban Mkwanywe* amesema mradi huo ni sehemu ya mradi mkubwa wa Usambazaji Maji kati ya Makongo na Mji wa Bagamoyo ambapo kwa Kata za *Wazo, Goba, Bunju na Mivumoni* zaidi ya *wateja wapya 15,000* wameunganishiwa huduma ya Maji
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa