-Kuongeza ufaulu wa wanafunzi katika Mkoa wa Dar es Salaam-Utekelezaji wa mkakati wa kuanzisha mfuko wa Barabara DSM
-Kuunda kikosi kazi cha kuwa na Muundo bora wa Jiji la DSM
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam CPA Amos Makalla ametaja vipaumbele vitatu (3) mahususi vya kutekeleza wakati akiahirisha kikao maalum cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa katika Ukumbi wa Anatoglo Mnazimmoja Ilala -Jijini Dar es Salaam
CPA Makalla amesema kuongeza ufaulu wa wanafunzi katika Mkoa wa DSM ni moja ya kipaumbele chake ambapo amewahakikishia wajumbe wa kamati ya ushauri ya Mkoa kuwa anaanza kuitisha Kikao kazi kitakachohusisha wadau wa elimu wote ambacho kitajadili kwa kina baadae kongamano kubwa la Elimu
Aidha CPA Makalla amebainisha kutokana na pendekezo la wajumbe wa kamati la kuwa na mfuko maalum wa barabara katika Mkoa, huku wakionyesha umuhimu na faida za mfuko huo CPA Makalla amesema Utekelezaji wa pendekezo hilo utatekelezwa mapema iwezekanavyo.
Vilevile CPA Makalla amesema kipaumbele kingine ni kuunda kikosi Kazi ambacho kitaketi na kitapitia kisha kuleta mapendekezo ya Muundo bora wa Jiji la Dar es Salaam
Sambamba na hilo CPA Makalla amewahakikishia wajumbe wa kamati ya Ushauri ya Mkoa kuwa Ushauri, maoni na mapendekezo ambayo wamewasilisha katika kikao hicho, yote yamepokelewa na yatafanyiwa kazi.
Kikao hicho cha Kamati ya Ushauri Mkoa (RCC) kimehudhuriwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa, Katibu Tawala Mkoa, Weheshimiwa Wabunge, Wakuu wa Wilaya, Mameya, Sekretarieti ya Mkoa, Wakurugenzi, Wakuu wa Taasisi na Mashirika ya Umma na wataalam wengine kutoka Halmashauri za Manispaa
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa