Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Amos Makala akiongea wakati wa kikao kazi katika ukumbi wa Anatoglo Jijini Dar es Salaam.
#Ataka jamii kuelimishwa na kuhamasishwa juu ya lishe bora.
#Wilaya zote za Mkoa wa Dar es Salaam kutenga bajeti katika masuala ya lishe na wataalamu wa lishe kutekeleza majukumu yao.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Amos Makalla wakati anafungua kikao kazi cha tathimini ya viashiria vya mkataba wa Lishe na mikakati ya Mkoa katika Kupambana na ugonjwa wa UVIKO -19.
Kikao ambacho kimehusisha Sekretarieti ya Mkoa wa Dar es Salaam, wakuu Wilaya zote, Makatibu tawala wa Wilaya, Wakurugenzi na wadau wengine katika ukumbi wa mikutano Anatoglo Jijini Dar es Salaam.
"Kwa uzoefu wangu katika maeneo niliyofanya kazi tatizo la lishe duni au udumavu halitokani na kutokosekana kwa chakula shida kubwa ni uelewa wa jamii katika ulaji wa mlo kamili" Alisema Mhe Makala
Mhe Mkuu wa Mkoa ameelekeza kwa wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi pamoja na wataalamu kutenga bajeti, kutoa elimu na kuihamasisha jamii katika ulaji wa mlo kamili au lishe bora.
Sambamba na hilo wataalamu wa lishe katika ngazi ya Wilaya zote watekeleze majukumu yao kwa kuzingatia taaluma zao.
Aidha mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt Rashid Mfaume akiwasilisha taarifa ya kikao hicho amesema Mkoa wa Dar es Salaam kwa sasa hakuna udumavu jitihada zaidi zitaelekezwa ili kuwa bora zaidi.
Imetolewa na:
OFISI YA HABARI NA UHUSIANO
MKOA WA DAR ES SALAAM
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa