- Asema Elimu itolewe Juu ya athari za Kelele na Mitetemo katika Jamii
- Taasisi za Dini zifanye kazi kwa karibu na Idara ya Ardhi na Mipango miji
- Asisitiza Umuhimu wa Kufuata Sheria za Mazingira
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Amos Makalla leo Septemba 28, 2021 amefungua Semina kwa Viongozi wa Dini Mkoa wa Dar es Salaam katika Ukumbi wa Millennium Tower Makumbusho, Dar es Salaam.
Akiongea katika warsha hiyo iliyoandaliwa na NEMC Mkuu wa Mkoa amewashuru Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kwa kuandaa Semina hiyo.
Mhe Makalla amebainisha wakati wa ziara yake ya Jimbo kwa Jimbo moja ya malalamiko aliyokuwa yakitolewa na wananchi ni pamoja na Kelele na Mitetemo na makelele mengi yanayolalamikiwa yanatoka sehemu za starehe kama vile mabaa na Nyumba za Ibada.
"Unakuta baa ipo katikati ya makazi na inapiga Mziki usiku kucha na nyumba za ibada nyingi zimejengwa pasipo kuzingatia taratibu za mipango miji hivyo kuleta athari za kiafya kwa jamii zinazunguka maeneo hayo " Alisema *Mhe Makalla*
Mkuu wa Mkoa amesema ziko athari nyingi za kiafya ikiwemo kukosa usikivu mzuri hatimaye kuwa kiziwi na msongo wa mawazo, Migogoro katika jamii na nyingine nyingi, hivyo sasa hatua sifuatazo lazima zifanyike kuinusuru Jamii .
Kwanza kabisa *Elimu* itolewe kwa Jamii juu ya athari za kiafya zinazotokana na makelele na Mitetemo.
Pili Taasisi za Dini zifanye kazi kwa karibu na Idara ya Ardhi na Mipango miji ili kuweza kubaini maeneo ambayo yanaruhusiwa kujenga nyumba za Ibada kwa mujibu wa taratibu za Mipango miji.
Aidha kwa kuwa sheria za Mazingira zipo ni wakati muafaka kila mtu Kufuata Sheria hizo ili kuondoa tatizo hilo katika Jamii.
Mhe Makalla amewataka Viongozi wa Dini na Wadau wengine wote baada ya Semina hii wakajitathimini kwa kina pamoja na kuwaelimisha wenzao na kuchukua hatua ili kumaliza tatizo hili la Makelele na Mitetemo katika Jamii.
|
|
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa