.
RC Makalla wa tatu kutoka kushoto akikagua eneo lillilovamiwa na wananchi wakijishulisha na uchimbaji wa kokoto Boko Kinondoni- Dar es Salaam
- Atoa Wiki moja kwa wavamizi kuondoka na kuondoa kokoto walizochimba.
- Akemea tabia ya wananchi kuvamia maeneo ya watu kiholela.
- Tamko la mkuu wa mkoa linafuatia Amri ya mahakama kutambua Kampuni ya Al Hushiim Investment ltd ambao ndio mmiliki halali.
- Aelekeza Jeshi la Polisi kuanza doria ya kulinda eneo Hilo Na kufikia tarehe 4/6/2022 Asionekane Mwananchi yeyote ili kampuni ijenge kiwanda cha Saruji
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla ameamuru kusimamia kwa Shughuli zote za uchimbaji wa madini kwenye eneo la mwekezaji Boko lililovamiwa na kutoa wiki moja kwa Wavamizi kuondoa mali na kokoto walizochimba Mara moja.
RC Makalla ametoa maelekezo hayo alipotembelea eneo Hilo lenye ukubwa wa hekta 70 ambapo tayari Mahakama ilishatoa haki kwa Kiwanda Cha Al Hushiim Investment ltd ambao ndio mmiliki halali.
Aidha RC Makalla amesema eneo Hilo ni mahususi kwaajili ya Shughuli za uchimbaji wa madini ambapo amepiga marufuku eneo kutumika Kama Makazi na kuelekeza kuanza kwa mchakato wa Kiwanda Cha saruji
Hata hivyo RC Makalla ameelekeza Jeshi la Polisi kuanza doria ya kulinda eneo Hilo kwa kushirikiana na walinzi wa kampuni hiyo ambapo amesema Magari yatakayoruhusiwa kuingia ni Yale yanayokwenda kuchukuwa mzigo pekee na sio uchimbaji.
Pamoja na hayo RC Makalla amemuelekeza Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni *Mhe. Godwin Gondwe* kufika kwenye eneo baada siku Saba kuanzia leo ili kujirudhisha.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa