-Awataka Wakuu wa Wilaya kusimamia vema utekelezaji wa viashiria 14 vilivyopo katika Mkataba huo
- Aagiza Mkataba huo kushuka kwenye kata mpaka mitaa
-Ataka changamoto zote kufanyiwa kazi Mara moja
-Amewasihi wazazi wote wenye watoto mashuleni kushirikiana na Kamati za shule ili kusaidia watoto kupata chakula
-RMO asema Dsm inaendelea kufanya vema pia katika lishe, chanjo ya UVIKO na kuchukua tahadhari ya Ebola
-Afisa Lishe wa Mkoa akiri Dsm kujipanga zaidi na kuhakikisha kila Halmashauri kufika asilimia 95
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makalla leo tarehe 26, Oktoba 2022 amesimamia zoezi la kusaini MKATABA wa Lishe kwa Wakuu wa Wilaya zote za Mkoa huo katika Ukumbi wa Anatoglo Jijini Dar es Salaam
RC Makalla amewataka Wakuu hao wa Wilaya kusimamia kikamilifu utekelezaji wa viashiria 14 vilivyopo katika Mkataba huo ambavyo ni pamoja na watoto kupatiwa chakula mashuleni, wakina mama wajawazito kuhudhuria clinic ipasavyo na kupatiwa madini joto, watoto kupatiwa matone ya vitamins A, Watoto wenye utapiamlo mkali kupatiwa Huduma vituoni, na utoaji wa fedha ipasavyo kwa ajili ya Afua za lishe
Mkuu wa Mkoa ameelekeza Mkataba huo kushuka kwenye kata mpaka kwenye mitaa kwani ni wa wananchi na kusisitiza kuwa Leo yeye ameanza na Wakuu wa Wilaya na wao wakafanye hivyo mpaka ufike mitaani
Aidha, RC Makalla ameagiza changamoto zote zikiwemo za utengaji wa fedha za afua za lishe, Utoajia wa Elimu ya Lishe kwa wananchi, chakula kwa wanafunzi zifanyiwe kazi Mara moja
Mhe. Makalla amewasihi wazazi wote wenye watoto mashuleni kushirikiana na Kamati za shule ili kusaidia watoto hao kupata chakula kwani chakula kinasaidia uwepo wa watoto mashuleni, kuongeza usikivu, ufanisi na kupunguza utoro kwa watoto Hali inayopelekea kuchochea ufaulu
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Dr. Rashid Mfaume amesema Dar es Salaam imeendelea kufanya vizuri katika suala la lishe, utoaji wa chanjo ya UVIKO 19 na kuchukua tahadhari ya Ugonjwa wa Ebola
Naye Afisa Lishe Mkoa Bi. Janeth Stanley amekiri kuendelea kujipanga zaidi ili kuhakikisha Halmashauri zote za Mkoa wa Dar es Salaam kila kiashiria kufikia asilimia 95 na sio chini ya hapo
Ikumbukwe kuwa Rais wa Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ndio muasisi wa Jambo hili toka akiwa Makamu wa Rais na amesaini na Wakuu wa Mikoa Mkataba wa Miaka 8 kwa sasa
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa