- Asema Mkoa umefanya vizuri zoezi la Sensa licha ya kuwa na idadi kubwa ya Wananchi.
- Dar es salaam inafanya zoezi la Sensa kwa umakini mkubwa ili kupata takwimu sahihi.
- Awataka Wananchi ambapo bado hawajahesabiwa kufika ofisi za Serikali ya mtaa au kupiga simu kupitia namba maalumu.
- Makarani wahimizwa kutuma taarifa kwa wakati.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amesema Mkoa huo umefanya vizuri kwenye zoezi la Sensa ya watu na Makazi ambapo mpaka asubuhi ya Leo August 30 taarifa zilizotumwa na Makarani wa sensa zinaonyeshazaidi ya Asilimia 94.3 ya Wananchi wamehesabiwa.
Akizungumza wakati wa kupokea taarifa ya mwenendo wa zoezi Hilo kwa Mkoa, RC Makalla amesema Makarani ambao bado hawajakamilisha kutuma taarifa wakituma taarifa zote ni dhahiri kuwa Mkoa utakuwa umefikia Asilimia 100.
Aidha RC Makalla amesema Mkoa huo unafanya Zoezi Hilo kwa umakini mkubwa ili kupata takwimu sahihi na za uhakika Kutokana na Mkoa huo kuchukuwa Asilimia 10-13 ya Wananchi wote wa Tanzania.
Ili kuhakikisha kila mmoja anahesabiwa, RC Makalla amewataka Wananchi ambao bado hawajahesabiwa kufika Ofisi ya Serikali ya mtaa na kuacha mawasiliano au kupiga simu kupitia namba maalumu zilizotangazwa kwa kila Wilaya ili aweze kufikiwa.
Pamoja na hayo RC Makalla amempongeza Kamisaa wa Sensa Anna Makinda kwa kuongeza siku ambapo pia amewapongeza Wakuu wa Wilaya kwa kusimamia Vizuri zoezi Hilo.
NAMBA ZA KUPIGA:
Kinondoni 0800110182
Ilala 0800110183
Temeke 0800110184
Ubungo 0800110185
Kigamboni 0800110186
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa