Mhe Amos Makalla akimkabidhi kablasha la mkataba mmoja wa kandarasi mzawa mara baada ya kusaini mapema leo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Amos Makalla ameshuhudia utiaji saini wa *mikataba takribani 41 kati ya TARURA na wakandarasi wazawa* 38 ya kutengeneza barabara na mitatu (3) ya miradi ya Maendeleo katika Mkoa wa Dar es Salaam.
Tukio hilo la kusaini Mikataba yenye thamani ya zaidi ya *bilioni 14* limefanyika leo katika ukumbi wa DMDP Ilala mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Akiongea wakati wa hafla hiyo *Mhe Amos Makala* kwanza kabisa ametoa Shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania *Mhe Samia Suluhu Hassan* kwa kuongeza kiasi cha fedha kutoka bilioni 21 hadi bilioni 40 kwa TARURA Mkoa wa Dar es Salaam.
Aidha amewataka wakandarasi ambao wamesaini mikataba leo kuifanya kazi hiyo *katika viwango, kwa wakati na kuzingatia thamani ya fedha* " Value for money"
"Mkifanya kazi vizuri katika awamu hii ya kwanza inawapa sifa ya kupata kazi awamu ya pili na mhandisi wa TARURA ameshasema utekelezaji wa kazi hii ni kwa awamu tatu" Alisema *Mhe Makalla*
Vilevile amewataka *TANESCO, TAN ROAD, DAWASA* kufanya kazi kwa pamoja pale TARURA wanapotekeleza miradi katika maeneo mbalimbali ndani ya Mkoa.
Pia amewataka kuzitunza barabara zinazojengwa katika Mkoa ikiwemo kuweka alama za barabarani kwa mfano sehemu ya watembea kwa miguu ijulikane, sehemu ambayo sio ya kupaki iwekwe ijulikane pia hili litasaidia wananchi kutotozwa faini za "wrong Parking" zisizo za lazima
Mhe Mkuu wa Mkoa pia ametoa onyo kali kwa vikampuni hewa vya kukusanya tozo au faini za "wrong Parking" kuacha mara moja kwa kuwa mamlaka husika zipo zinazotakiwa kufanya kazi hiyo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa