RC Makalla wa katikati kiti cha mbele pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama wakifuatilia maelekezo ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kasim Majaliwa kwa njia ya Mtandao "Video Conference"
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Amos Makalla, leo Machi 14,2022 ameshiriki kikao Kazi cha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kasimu Majaliwa kwa njia ya Mtandao "Video Conference" kilichofanyika katika ukumbi wa TTCL Samora Ilala Jijini Dar es Salaam.
Kikao kazi hicho kimelenga kupokea maelekezo kutoka kwa waziri Mkuu na kukumbushana majukumu ya kila siku yanayosimamiwa na wakuu wa Mikoa Tanzania Bara. Miongoni mwa maelekezo ya Waziri Mkuu kwa wakuu wa Mikoa ni, Kusimamia vizuri ukusanyaji na matumizi ya mapato, Ulinzi na Usalama wa watu na mali zao, Hali ya Uchumi, kama vile udhibiti wa mfumko wa bei za bidhaa, Usimamizi wa miradi ya maendeleo kama vile Elimu, Barabara, Maji, Nishati ya Umeme .
Hata hivyo amewataka kuhakikisha Umma unahabarishwa kila kitu kinchotekelezwa katika Mkoa pia kusimamia eneo la machinga kwa kuwapanga vizuri,pasipo kutumia nguvu huku akipongeza Mkoa wa Dar es Salaam kwa kufanya vizuri katika kuwapanga vizuri wamachinga vilevile kuhakikisha zoezi la Anwani za makazi linafanyika kwa weledi na kuhakikisha ifikapo may, 31,2022 liwe limekamilika.
Aidha Washiriki wengine walioambatana na Mkuu wa Mkoa ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Ndg Hassan Rugwa, Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe Ally Happi , Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa pamoja na viongozi wa Chama cha Mapinduzi
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa