- Ni shule ya Wasichana ya Kisasa na kipekee Tanzania, Kata ya Kwembe Jimbo la Kibamba.
- Amshukuru Rais samia kutoa fedha Bilioni 3 Na Mpaka Sasa Ujenzi umefikia asilimia 86 na itaanza kupokea Wanafunzi Mwezi Julai mwaka huu.
- Aelekeza Ujenzi wa Uzio kuzunguka shule Kuanza mara Moja.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam CPA, Amos Makalla ameridhishwa na Maendeleo ya ujenzi wa Shule mpya ya Bweni kwa wasichana Mkoani humo inayojengwa Kata ya Kwembe Wilaya ya Ubungo na kumshukuru Rais Dkt, Samia Suluhu Hassan kwa kutoa zaidi ya Shilingi bilioni 3 kwaajili ya shule hiyo ya kipekee nchini.
Akizungumza wakati wa Ziara ya kukagua Maendeleo ya ujenzi huo, CPA Makalla ameelekeza Ujenzi wa Ukuta kuzunguka shule hiyo Kuanza mara Moja Ili itakapoanza kutumika wanafunzi wawe kwenye mazingira salama.
Aidha CPA, Makalla amesema ifikapo Mwezi Julai mwaka huu shule hiyo itaanza kupokea Wanafunzi kwaajili ya muhula wa masomo na kumuelekeza Mkandarasi kuharakisha Ujenzi.
Ujenzi wa Shule mpya ya wasichana ya Mkoa wa Dar es salaam inayojengwa Kata ya Kwembe inahusisha Ujenzi wa madarasa 12, Mabweni 5, Bwalo, jengo la utawala, jiko, Maabara na miundombinu mingine.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa