- Asema utaharakisha utatuzi wa migogoro
- Awaomba mawakili kushawishi wateja wao kwa kesi zinazohitaji usuluhishi
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam CPA Amos Makalla ameipongeza Mahakama kwa utatuzi wa migogoro kwa njia ya usuluhishi, pongezi hizo amezitoa leo wakati akitoa salamu za Mkoa katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya sheria nchini Kanda ya Dar es Salaam katika viwanja vya Mahakama ya Kisutu Jijini Dar es Salaam
RC Makalla amesema utatuzi migogoro kwa Usuluhishi utaharakisha utatuzi wa migogoro kwa kuwa migogoro mingi itatatuliwa na kumalizwa katika ngazi hiyo pasipo kupelekwa mahakamani hivyo kuchagiza kauli Mbiu ya kuwa na uchumi endelevu.
Aidha Mhe Amos Makalla amewaomba Mawakili kushawishi wateja wao kwa kesi zinazohitaji usuluhishi ili kuweza kuokoa muda, gharama na usumbufu wa nenda rudi mahakamani ambapo migogoro itamalizwa mapema na kutoa fursa kwa wananchi kuendelea na majukumu yao ya kila siku ya kujiletea kipato na kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa Ujumla.
Hata hivyo CPA Amos Makalla ametoa uzoefu wake kuwa wananchi wemekuwa wakiamini Mhe Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Mkuu wa Mkoa, wakuu wa Wilaya wanauwezo wa kufuta hukumu ya mahakama ambapo sio kweli, ukweli ni kwamba mhimili wa Mahakama hauingiliwi na mtu yoyote kama hujaridhika unapaswa kukata rufaa ngazi ya juu ya mahakama hivyo ni vizuri kuendelea kutoa elimu ya sheria kwa Umma ili wapate uelewa wa sheria.
RC Makalla amesema Serikali ya Mkoa itaendeleza mshikamano na ushirikiano na Mahakama kwa masilahi mapana ya Wananchi
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa