Waheshimiwa Madiwani wa Manispaa ya Kinondoni wakati wa Baraza Maalum katika Ukumbi wa Manispaa hiyo Jijini Dar es Salaam
- Awataka Madiwani kusimamia Viizuri Halmashauri ili kulinda hati safi waliyopata.
- Awaelekeza kufanyia kazi hoja zote za CAG na kuzifunga ili zisijirudie.
- Ataka Maoni na mapendekezo ya wakaguzi wa ndani yafanyiwe kazi.
- Baraza la Madiwani laahidi kufanyia kazi maelekezo yote.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amezielekeza Halmashauri za Manispaa ya Ubungo na Kinondoni kuhakikisha wanafanyia kazi Maoni na mapendekezo yaliyotolewa na Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi wa hesabu za Serikali CAG ili kuhakikisha wanaendelea kupata hati safi.
RC Makalla ametoa maelekezo hayo nyakati tofauti wakati wa Vikao maalumu vya Baraza la Madiwani Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo na Kinondoni kilichoketi kupitia Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi wa hesabu za Serikali CAG.
Akiwa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, RC Makalla amewaelekeza Madiwani kuisimamia vizuri Halmashauri hiyo kwa kuhakikisha hoja zote za CAG zinafanyiwa kazi kwa wakati, kufungwa na kuweka Mikakati ya kuhakikisha hazijirudii
Aidha RC Makalla ameelekeza Halmashauri hiyo kutafuta ufumbuzi wa uendeshaji wa timu ya mpira wa miguu ya KMC iliyo Chini ya Halmashauri Kutokana na taratibu za uendeshaji kupeleka kuibuka kwa hoja nyingi inapokuja suala la Ukaguzi.
Kuhusu mashauri ya kesi zilizopo Mahakamani zinazohusisha zaidi ya Shilingi Bilioni 15, RC Makalla amesisitiza Halmashauri kupitia wanasheria kufanya uhakiki ili kuziondoa kesi hizo Mahakamani na kuzimaliza kwa njia ya maridhiano ya pamoja Kutokana na mashauri kuchukuwa muda mrefu na kuigharimu Serikali.
Hata hivyo RC Makalla ameshiriki baraza la Madiwani Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo ambapo amepongeza Halmashauri hiyo kwa kupata hati safi licha ya uchanga wake.
Pamoja na hayo RC Makalla ameendelea kusisitiza Mkazo kwenye Zoezi la Anuani za Makazi, Sensa ya watu na Makazi, kudhibiti Ufanyaji biashara holela na Usafi.
RC Makalla akisalimiana na Diwani wa Kawe Mhe Muta Rwakatare baada ya kumaliza kikao cha Baraza Maalum Manispaa ya Kinondoni
Waheshimiwa Madiwani wa Manispaa ya Ubungo wakati wa Baraza Maalum katika Ukumbi wa Manispaa hiyo Jijini Dar es Salaam Mapema leo
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa