Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe.Amos Makalla leo amefungua tawi la Bank ya NBC Kigamboni ikiwa ni sehemu ya Mkakati wa bank hiyo kusogeza huduma Kibenki karibu na Wananchi.
Akizungumza wakati wa ufunguzi huo, RC Makalla ametoa wito kwa bank hiyo kuzingatia mahitaji ya Wateja,kubuni huduma za kuvuta wateja wengi Zaidi na kuendelea kufungua matawi mengi Zaidi.
Aidha RC Makalla amepongeza Bank hiyo Kongwe nchini kwa kulinda hadhi yake na kubaki kwenye ubora uleule Tangu mwaka 1967 ilipoanzishwa.
Pamoja na hayo RC Makalla amehimiza bank hiyo kuendelea kutoa Mikopo yenye masharti nafuu kwa Wafanyabiashara na wajasiriamali ili kukuza mitaji ya Wafanyabiashara kuinua Uchumi wa Taifa.
Uzinduzi wa Tawi la NBC Kigamboni linafanya bank hiyo kufikisha *Matawi 16 Mkoa wa Dar es salaam, Matawi 47 Nchi nzima, ATM 180 na Bank kuwa na Mtaji wa fedha takribani Shilingi trilioni 2.7.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa