- Ni Vitanda 108, Meza 38 na Vyuma161 kwaajili ya majeruhi wa Ajali.
- Avigawanya kwa kila Halmashauri ya Mkoa
- Ampongeza Rais Samia kwa kudumisha ushirikiano wa kidiplomasia baina ya Tanzania na Ujerumani.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Amos Makalla leo amepokea Vifaa vya Afya ikiwemo Vitanda vya Wagonjwa, Meza za Wagonjwa na Vyuma vya kusaidia majeruhi wa Ajali kutoka Jiji la Hamburg Ujerumani ambapo Baada ya kupokea amevigawa kwa Halmashauri zote tano za Mkoa.
Akitoa mgawanyo wa Vifaa hivyo, RC Makalla amesema Jiji la Dar es salaam wamepata Vitanda 20, vyuma 32 vya Wagonjwa wa Ajali na meza 7,Halmashauri ya Kigamboni Vitanda 28, meza 10 na vyuma 33 vya Wagonjwa wa Ajali na Halmashauri ya Kinondoni Vitanda 20, meza 7 na vyuma 32 vya Wagonjwa wa Ajali.
Aidha RC Makalla amesema Halmashauri ya Temeke imepata Vitanda 20, Meza 7 na vyuma 32 vya Wagonjwa wa Ajali huku Halmashauri ya Ubungo wakipata Vitanda 20, bedside 7 na vyuma 32 vya Wagonjwa wa Ajali ambapo ameelekeza Vifaa hivyo kutumika vizuri.
Pamoja na hayo RC Makalla amesema msaada huo umekuja wakati muafaka ambapo tayari Rais Samia Suluhu Hassan amefanya maboresho makubwa sekta ya Afya kupitia Ujenzi wa Hospital, Vituo vya Afya na Zahanati na Vifaa hivyo vitakwenda kuongeza Nguvu sehemu hizo.
Hata hivyo *RC Makalla* ameelekeza *Kontena tatu Kati ya sita za Vifaa hivyo* ambazo bado zipo bandarini *zikombolewe* kwa wakati ili *lengo la kutolewa kwa msaada huo liweze kutimia
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa