- Apongeza na kusifu Jitihada za Rais Samia kuifungua Tanzania
- Awashukuru Wajerumani- Humburg na kusema huo ni msaada wa Awamu ya kwanza, wa Awamu ya Pili kuja
- Ataja Vifaa hivyo na kupelekwa Hospitali za Wilaya zote za Dsm
- Aomba Vifaa hivyo kutunzwa ili vidumu
-RMO Ataja mgao wa kila Hospitali ya Wilaya DSM
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makalla leo tarehe 4 February 2022 amepokea Msaada wa Vifaa Tiba vyenye thamani ya Shilingi Milioni 205 kutoka Ujerumani - Humburg
Mhe. Makalla amepongeza na kusifu Jitihada kubwa zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan za kuifungua Tanzania Kimataifa ambapo imepelekea Tanzania kupokea misaada mbalimbali ikiwemo hiyo ya Vifaa Tiba
Mkuu wa Mkoa ametaja Vifaa hivyo kuwa ni pamoja na Vitanda 108 na Meza za Pembeni 72 ambavyo vinaenda kupunguza Msongamano Hospitalini na kutatua changamoto mbalimbali Hadi Kuboresha Hospitali za Mkoa wa Dar es Salaam
Hata hivyo Mhe. Makalla amewashukuru Wajerumani- Humburg na kusema huo ni msaada wa Awamu ya Kwanza ambapo wa Awamu ya Pili unatarajiwa kufika hivi karibuni ukiwa na "Container 9" zenye Meza 152 na Vitanda 151
Aidha Mkuu wa Mkoa ameomba kutunzwa kwa Vifaa hivyo ili vidumu kwa vizazi hata vizazi
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Rashidi Mfaume ametaja mgawanyo wa Vifaa hivyo katika Hospitali za Wilaya za Dar es Salaam kuwa ni pamoja na Kigamboni Vitanda 24, Makabati 16, Kinondoni Vitanda 21,Makabati 14, Temeke Vitanda 21,Meza 14, Jiji Vitanda 21, Meza 14 na Ubungo Vitanda 21 ,Meza 14
Hafla hiyo imehudhuriwa na Katibu Tawala wa Mkoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, Rmo, Meya wa Kigamboni, Kamati ya Amani na Watumishi wa Kigamboni
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa