- Awakutanisha Pamoja Jumuiya ya wafanyabishara na Watendaji wa Serikali DSM wakiwemo TRA, Bandari, Uhamiaji na Jeshi la polisi
-Aongoza mjadala wa kuweka mazingira bora ya Kibiashara na Uwekezaji DSM, Atoa maagizo 7 ya Utekelezaji wa makubaliano yaliyofanyika
-Ampongeza Rais Samia kwa kuvunja rekodi kupandisha mishahara ya watumishi kwa 23.3%
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Amos Makalla leo Mei 16, 2022 amefanya kikao Kazi kwa kuwakutanisha pamoja Jumuiya ya wafanyabishara DSM pamoja na Watendaji wa Serikali na wadu wengine kwa lengo la kupokea Changamoto zao na kuweka mazingira rafiki ya Kibiashara na Uwekezaji kwa Masilahi Mapana ya Mkoa na Taifa kwa Ujumla
Kikao ambacho kimefanyika katika Ukumbi wa Mikutano Anatoglo Mnazimmoja Ilala-Jijini Dar es Salaam.
Akiongea wakati wa kikao hicho RC Makalla amesema pamoja mambo mengine anayosimamia Mapato ni kipaumbele kwake na namna mojawapo ya kupandisha mapato ni pamoja na kuweka mazingira rafiki ya Kibiashara pasiwepo na kero zinazokwamisha utendaji wa biashara.
Aidha RC Makalla ameyataja maeneo Makuu manne ya kero ambayo ni miongoni mwa kero zilizowasilishwa kwake na Jumuiya ya wafanyabishara DSM.
Miongoni mwa kero hizo ni Ukamataji wa mizigo ya wafanyabishara hasa wa nje kero iliyoelekezwa TRA na Jeshi la polisi, Utoaji wa muda wa Vibali (Vissa) kwa wafanyabishara wa nje umekuwa ni siku 7 ambao hautoshelezi Kibiashara angalau ungesongezwa kuanzia siku 30-90
Vilevile Kero ya Ucheleweshaji wa mizigo Bandari na makadirio ya kodi kwa wafanyabishara sio rafiki
Hata hivyo Mkuu wa Mkoa alitoa nafasi kwa Watendaji wa Serikali kutoa majibu ya kero zilizoelekezwa katika Mamlaka zao hususani kero zilizoko ndani ya uwezo wa taasisi kwa lengo la kuweka mazingira rafiki ya Wafanyabishara DSM.
RC Makalla baada ya kusikiliza majibu yaliyotolewa akatoa maagizo 7 kama ifuatavyo: Majibu yote yaliyo tolewa kwa Upande wa TRA, Bandari, Uhamiaji, yawekwe katika maandishi yafike Ofisini kwake Jumatano Saa 5:00 Asubuhi, Mkoa uwe tayari kimkakati kuhakikisha unaendelea kuchangia pato la taifa kwa kiwango kikubwa huku akitaka kuundwa kwa kamati ya kushughulikia masuala ya biashara itakayoongozwa na katibu Tawala Mkoa
Vilevile mabaraza ya wafanyabishara yafanyike katika Wilaya zote za Mkoa wa Dar es Salaam, Mamlaka za Udhibiti biashara kama Osha, Zimamoto, TBS na zingine kutoa nafasi nzuri na rafiki kwa wafanyabishara kufanya kazi zao, Mamlaka ya Bandari Tanzania kuwaandikia barua "Shipping Line" kufanya kazi kwa weledi mzigo ukiingia mara moja kupelekewa Bandari kavu, Uhamiaji kupeleka mapendekezo ya namna ya kuboresha utoaji wa "Vissa" kwa Kamishna Jenerali
Kwa Upande Ushuru wa huduma "Service Levy" RC Makalla ameagiza katibu Tawala ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati kuja na mapendekezo ya ni kifanyike
Sambamba na hilo Mkuu wa Mkoa wa DSM amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kusikia kilio cha Siku nyingi cha watumishi wa Umma na kupandisha mishahara kwa alimia 23.3 na ametoa Rai kwa watumishi wote kutekeleza wajibu wao kwa kufanya kazi kwa bidii
Mhe Amos Makalla siku ya Jana Mei 15, 2022 ametimiza mwaka mmoja toka ateuliwe na Mhe Rais huku Mkoa ukiwa na mafanikio lukuki katika nyanya za Mapato, Ulinzi na Usalama, Kuwapanga vizuri Wamachinga, Kampeni Usafi , Usikilija wa kero za wananchi, Usimamizi wa kiwango cha juu miradi ya maendeleo, na Ukamilishaji kwa wakati Ujenzi wa madarasa na Anwani za Makazi
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa