- Awataka wananchi wa MVUHA, DUTUMI, TULO MOROGORO vijijini kuondoa haraka mifugo katika vyanzo vya maji ikiwemo mto Ruvu
- Kamati za ulinzi na Usalama Wilaya za Bagamoyo, Kibaha na Morogoro zatakiwa kukutana haraka kudhibiti mifugo na wachepushaji maji wachache waliobaki
- Awaomba wanachi wa Mkoa wa Dare es Salaam kuendelea kuwa watulifu wakati serikali ikiendelea kuchukua hatua za haraka za kufufua visima 197 ili kuongeza maji
- Asema kazi ya kuingiza maji lita milioni 70 Kutoka KIGAMBONI imekamilika
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe Amos makalla leo Novemba 3,2022 ameongoza ukaguzi wa Mto Ruvu pamoja na mito yote inayoingiza maji katika Mto Ruvu ziara hiyo amehusisha vyombo vya ulinzi, kaimu mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe Sara msafiri na watalaam wa bonde Mto Ruvu
Ukaguzi huo umefanyika katika mto Ruvu kuanzia wilaya Nagamoyo, Kibaha na morogoro vijijini Kwa kuangalia vyanzo vya mito ya Mgeta, Mvuha na Dutumi
Aidha katika ukaguzi huo wameona maji yameendelea kupungua kutokana naa ukame pia baadhi ya maeneo yakiwa na mifugo.
Hata hivyo RC Makalla amewataka wananchi wa Durumi na Mvuha kuondoa haraka mifugo katika vyanzo vya maji ikiwemo Mto Ruvu
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa