-Asema Mkoa umepokea Bilioni 12 na milioni 360 kwa ajili ya Ujenzi huo
- Aelekeza Ujenzi wa vyumba vya madarasa ufanyike kwa Force Account
- Ataka Ujenzi kuzingatia Ubora, thamani ya pesa na kukamilika kwa wakati
RC Makalla amesema hayo leo Octoba 7,2022 katika kikao chake na Walimu Wakuu wa Shule za Sekondari DSM, Ukumbi wa Arnatoglo Mnazimmoja, ambacho kilihudhuliwa na Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na Maafisa Elimu, na Sekretarieti ya Mkoa ikiongozwa na Katibu Tawala wa Mkoa huo Bi Rehema Madenge
Mhe Makalla amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutekeleza Ilani ya CCM kwa vitendo kufuatia Mkoa huo kupewa kiasi cha Bilioni 12 na milioni 360 ambazo zimeelekezwa katika Ujenzi wa vyumba vya madarasa 618 sawa na shule 108
Aidha RC Makalla ameelekeza kujenga Madarasa ya mfano kwa kutumia Force Account huku akisisitiza pesa hizo zikatumike kujenga madarasa na sio kulipa fidia.
Vilevile Mhe Makalla amewataka kusimamia vizuri zoezi hilo kwa kuzingatia thamani ya pesa na Ubora bila kusahau kazi ifanyike kwa wakati ifikapo Novemba 30,2022 Ujenzi uwe umekamilika.
Sambamba na hilo RC Makalla amesema amepokea migogoro 41shule za Sekondari na 25 Shule za msingi ya uvamizi wa Ardhi maeneo ya shule hivyo amewataka Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi kwenda kumaliza migogoro hiyo kwa kuyatembelea maeneo hayo, kuyakagua, Kuyajua vizuri maeneo hayo na kuweka mipaka
RC Makalla ameelekeza migogoro yote ikashughulikiwe kwa ufanisi na apatiwe taarifa ya Utekelezaji wa zoezi hilo
Kwa Upande wa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Godwin Gondwe kwa niaba ya wakuu wa Wilaya wengine amemhakikishia Mkuu wa Mkoa kwenda kutekeleza maagizo yake aliyotoa ili ifikapo Januari 2023 wanafunzi waingie katika vyumba hivyo vya madarasa
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa