- Asema uamuzi huo umewasaidia wafanyabiashara kufanya Biashara Kwa uhakika
- Zaidi ya 95% ya mafuta Ya kula hupita bandari ya mbweni.
- Aiagiza Mamlaka ya Bandari TPA Na TARURA kuandaa michoro, gharama Za barabara Na miundombinu ya bandari
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla ameelekeza Mamlaka ya Bandari kufanya Maboresho ya Miundombinu ya Bandari ndogo ya Mbweni Baada ya Rais Samia kurasimisha rasmi Bandari hiyo.RC Makalla ametoa maelekezo hayo wakati wa ziara kwenye Bandari hiyo ambapo amewataka TPA Na TARURA kuandaa michoro, gharama Za barabara Na miundombinu ya bandari hiyo ili biashara zifanyike pasipo usumbufu.
Aidha RC Makalla amemshukuru na kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa uamuzi wake wa kurasimisha Bandari hiyo Baada ya muda mrefu kutumika Kama Bandari bubu na kusababisha Serikali kukosa Mapato.
Hata hivyo RC Makalla amesema Asilimia 95 ya Mafuta ya kula yanapita Katika bandari hiyo hivyo ni lazima maboresho yafanyike ambapo ametoa wiki moja kwa Mamlaka ya Bandari kuweka kibao Cha kuonyesha Bandari hiyo.
Katika ziara hiyo RC Makalla amepokea changamoto mbalimbali kutoka kwa Wafanyabiashara wanaotumia Bandari hiyo na kuahidi kuzipatia ufumbuzi wa haraka.
Pamoja na hayo RC Makalla ametoa wito kwa Wafanyabiashara wanaotumia Bandari hiyo kutokumuangusha Rais Samia kwa kuhakikisha wanalipa mapato na kufuata sheria, kanuni na taratibu.
Ikumbukwe kuwa Bandari ndogo ya Mbweni imerasimishwa rasmi tarehe 06/ 05/2022 na Rais Samia Suluhu Hassan na Sasa inatoa huduma Kwa mujibu wa sheria
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa