- Zaidi ya shilingi bilioni 231 zimetolewa kujenga Barabara ya Km 23 kutoka katikati ya mji kuelekea Gongolamboto.
- Amuelekeza Mkandarasi kuhakikisha mwezi March mwakani mradi unakamilika.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam CPA. Amos Makalla ametembelea Mradi wa ujenzi wa Barabara ya mwendokasi BRT Awamu ya tatu kutoka katikati ya mji kuelekea Gongolamboto na kumtaka Mkandarasi wa kampuni ya Sinohydro kuhakikisha kazi inakamilika ifikapo Mwezi March mwakani.
RC Makalla amesema mradi huo unagharimu shilingi bilioni 231 ikihusisha ujenzi wa Km 23, Vituo 32, Karakana moja, Vituo vikubwa vinne na Daraja kubwa moja.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo RC Makalla amesema kukamilika kwa mradi itasaidia kurahisisha shughuli za usafiri kwa Wananchi ambapo amempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuifungua Dar es salaam.
Katika ziara hiyo RC Makalla amewaelekeza TANROAD kufanya maamuzi haraka ya wapi ijengwe karakana kutokana na eneo walilopanga kujenga kuwa na mkataba na mwekezaji atakaejenga kiwanda Cha Vioo kitakachotoa Ajira kwa zaidi ya vijana 6,000 hivyo amewataka kutafuta eneo lingine watakalolipa watu fidia.
Mradi wa ujenzi wa Barabara ya mwendokasi kuanzia Awamu ya kwanza mpaka Awamu ya Sita itahusisha zaidi ya Km 150 ambapo mpaka Sasa Awamu ya kwanza umekamilika, Awamu ya pili Mbagala inategemewa kukabidhiwa Mwezi March mwaka huu na Sasa Awamu ya tatu kuelekea Gongolamboto Ujenzi wake umeanza mwezi January mwaka huu.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa