-Rais samia ameelekeza Kujengawa Soko la Jangwani ambalo litakuwa la Wamachinga na Stendi ya Mabasi kuwepo
-Aidhaa, Rais Samia ataka masoko ya Wamachinga kujengwa kila Wilaya
- Awataka waliokosa maeneo kujitokeza na kupangiwa Mara moja
-Ataka waliopanga barabarani Mtaa wa Kongo kuondoka Mara moja
-DC Ilala kwa kushirikiana na RPC na OCD waahidi kuyalinda maeneo yote
-Balozi wa Usafi Dsm Harmonize Aomba wamachinga kushirikiana Na serikali
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makalla leo tarehe 27 Februari 2022 ameendelea na Kampeni yake ya SAFISHA PENDEZESHA DAR ES SALAAM inayofanyika kila mwisho wa Mwezi ambapo leo alikuwa katika Wilaya ya Ilala - Mtaa wa Msimbazi na Tabata Bima Mpakani
*Mhe. Makalla* amewaeleza wananchi wa Ilala kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania *Mhe.Samia Suluhu Hassan* tayari ameshaidhinisha kiasi Cha Shilingi *Bilioni 26* ili Kujenga soko la Kariakoo na Ujenzi unaendelea aidha tayari ameelekeza Kiasi Cha *Bilioni 6 kutumika katika Kujenga Soko la *Jangwani* ambalo litakuwa la Wamachinga na litakuwa na Stendi aidha Wamachinga wameshirikishwa katika michoro
Hata hivyo Mkuu wa Mkoa ameongeza kuwa Rais wetu mpendwa hakuishia hapo ametaka kila Wilaya ya Dar es Salaam kujengwa Masoko ya Wamachinga ili kupunguza adha ya kila mtu kuja mjini
Wakati huo huo RC Makalla amewataka waliokosa maeneo kujitokeza na kupangiwa kwani maeneo bado yapo na watakapopangwa wakae katika maeneo yao waliyopangiwa
Vile vile Mkuu wa Mkoa amewata wote waliopanga barabarani Mtaa wa Kongo kuondoka Mara moja kwani Sheria Kali dhizi Yao zitachukuliwa kwa watakaokaidi
Kwa upande wake DC wa Ilala Mhe. Ludigija amesema yeye kwa kushirikiana na RPC na OCD wameahidi kuyalinda maeneo yote yaliyoachwa na Wamachinga kwa masaa yote
Naye Balozi wa Usafi Dsm Harmonize ameomba Wamachinga kushirikiana na Serikali kwani Viongozi wa Serikali wanaposema wamachinga wasipange bidhaa barabarani basi watii na kutekeleza kwa manufaa yao
Kampeni hiyo ya SAFISHA PENDEZESHA DAR ES SALAAM imehudhuliwa na DC ILala, Meya, Madiwani, NMB, Wakuu wa Idara- Ilala, Viongozi wa Wamachinga, Balozi wa Usafi, Wafanyabiashara, Jogging Clubs, na Bodaboda
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa