- Amshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za kutekeleza mradi huo
-Apongeza Manispaa ya Temeke kwa utekelezaji wa mradi pamoja na Changamoto ya uhaba wa Ardhi
-Ataka Ujenzi ukamilike kwa wakati kwa viwango na ubora
-Awataka Viongozi wa Serikali ya Mitaa kuitisha mikutano ya hamasa kuhamasisha watoto kwenda Shule
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Amos Makalla leo ametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa vyumba ya madarasa ya Ghorofa 32 na Msambao 24 katika Shule ya Sekondari Lumo Wilaya ya Temeke Jijini Dar es Salaam.
Akiwa katika eneo hilo Lumo-Temeke RC Makalla amemaliza mgogoro wa Ardhi na kuwataka wananchi kuendelea kushirikiana na Serikali ili kujiletea maendeleo, amesema eneo hilo ni la Serikali wananchi wataje majina ya walio wauzia maeneo hayo ili Serikali iwachukulie hatua za kisheria.
Vilevile ameagiza kujengwa kwa uzio kuzunguka eneo la shule kuepuka uvamizi na Viongozi wa ngazi za Kata na Mitaa kuyalinda maeneo ya Umma yaliyotengwa yatumike kwa kusudio lake
Hata hivyo RC Makalla amemshukuru Rais Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa dhamira yake ya kuboresha miundo mbinu ya elimu Nchini hususani Mkoa wa DSM na kuwataka Viongozi na wana DSM kutembea kifua mbele.
Aidha RC Makalla amepongeza Manispaa ya Temeke kwa kukabiliana na uhaba wa Ardhi kufikia maamuzi ya Ujenzi wa vyumba vya madarasa ya Ghorofa 32 na kuongeza fedha kutoka mapato ya ndani milioni 500 na Ujenzi unaendelea kwa kasi kubwa.
Hata hivyo Mhe Amos Makalla amewataka kukamilisha kwa wakati kwa kuzingatia thamani ya fedha, Viwango na Ubora
Sambamba na hilo RC Makalla amewataka Viongozi wa Mitaa kufuatia juhudi kubwa zinazofanywa na Mhe Rais Dkt Samia kuboresha miundo mbinu ya elimu wao kama Viongozi kuitisha mikutano ya hamasa kuhamasisha watoto kwenda Shule na Kamati za ulinzi na usalama zisimamie hilo
Mwisho Halmashauri ya Manispaa ya Temeke pekee imepokea fedha kiasi cha Tshs Bilioni 4.1 kwa ajili ya Ujenzi wa vyumba vya madarasa 207 ambayo vinatarajiwa kutumika rasmi Januari 2023
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa