-Atoa siku 60 Wananchi waliovamia Kuondoka
- Aelekeza Uongozi wa Simba Sports Club kuanza kujenga uzio kuzunguka kiwanja hicho leo Septemba 14
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Amos Makalla leo Septemba 14, 2022 amemaliza mgogoro wa Ardhi katika kiwanja namba 229 Kinachomilikiwa na Simba Sports Club Bunju B Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
RC Makalla baada ya kuzuru eneo la kiwanja amepata wasaa wa kujionea mipaka na Wananchi takribani 9 ambao wamevamia na kujenga katika eneo hilo.
Aidha RC Makalla amewataka wananchi waliovamia katika kiwanja hicho ndani ya siku 60 kuanzia leo Jumatano Septemba 14, 2022 kujipanga kuondoka mara moja kwa kuwa eneo hilo ni mali halali ya Simba Sports Club ndio wenye hati miliki.
" Uvamizi wa Ardhi ni ualifu kama ulivyo ualifu mwingine wowote ambapo anayetenda kosa anastahili kuchuliwa hatua za kisheria " Alisema *RC Makalla
RC Makallaameelekeza Uongozi wa Simba Sports Club kuanza mara moja ujenzi wa uzio kuzunguka kiwanja hicho kama walivyokusudia huku akimuagiza Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni *Mhe Godwin Gondwe kumuagiza OCD kusimamia Ulinzi na Usalama katika eneo hilo katika Kipindi chote cha Utekelezaji wa zoezi hilo.
Hata hivyo RC Makalla ametoa Rai kwa Simba Sports Club kuendeleza uwekezaji wa kiwanja hicho kwa kuwa ni fursa ya kibiashara kwa wakazi wa Bunju Wilaya, Mkoa na Taifa kwa Ujumla
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa