-Awataka kuendelea kuchapa kazi kwa masilahi mapana ya Wananchi hususani wakazi wa DSM
-Apongeza namna miradi inavyotekelezwa DSM Ataka TANROAD kuangalia namna bora ya kutekeleza miradi pasipo kuwepo kwa KERO za foleni au kufunga kwa baadhi ya Barabara
- Asisitiza TANESCO kuboresha huduma maeneo ya pembezoni na na Utoaji taarifa kwa umma
-Aendelea kutoa wito Taasisi za Umma kusimamia USAFI na kuyalinda maeneo yao dhidi ya biashara holela
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Amos Makalla leo Machi 09, 2022 amekutana na Watendaji wakuu wa TANROAD, TANESCO, DAWASA na TARURA na kufanya nao kikao kazi katika Ofisi yake Ilala- Dar Es Salaam.
RC Makalla amewataka kuendelea kuchapa kazi kwa kuwa Taasisi zao zinagusa maisha ya Wananchi moja kwa moja, licha yakuwa wamekua wakifanya kazi vizuri wanatakiwa kuongeza jitihada ili kuleta ufanisi zaidi.
Mkuu wa Mkoa amegusia maeneo ambayo yamekuwa na Changamoto kwa mfano TANROAD katika Utekelezaji wa miradi hasa ya Mwendokasi kumekuwa na malalamiko ya foleni lakini pia kufungwa kwa Barabara nyakati fulani hali inayopelekea kudidimiza shughuli zingine za kiuchumi, hivyo ni wajibu wa Viongozi husika kulifanyia kazi jambo hilo ikiwezekana baadhi ya shughuli za Ujenzi wa Barabara zifanyike usiku.
Aidha RC Makalla amewataka TANESCO kuboresha Utoaji wa huduma za umeme hasa maeneo ya pembezoni mwa Mkoa wa DSM kwa mfano chanika, Vilevile waimarishe mifumo ya Mawasiliano kwa Umma ikiwemo Utoaji taarifa kwa wateja pale kunapokuwa na Changamoto ili wananchi wajue.
Hata hivyo RC Makalla amewataka DAWASA na TARURA kuainisha miradi mipya inayotekelezwa katika maeneo mbalimbali ya Mkoa ili aweze kutembelea kuona namna miradi hiyo inavyotekelezwa.
Sambamba na hilo Mhe Makalla amezitaka Taasisi hizo kuendelea kusimamia USAFI ikiwemo kuyalinda maeneo yao, amesisitiza kwa muda mfupi tumeona matokeo Jiji la DSM limekuwa la sita Afrika kwa Usafi hivyo uwezekano wa kufanya Vizuri zaidi upo kama kila mmoja atashiriki kwa nafasi yake "SAFISHA PENDEZESHA DAR ES SALAAM" Usafi ni Mimi na wewe.
Kikao kazi hicho kimehudhuriwa na Wataalam kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wakiongozwa na Katibu Tawala wa Mkoa Ndg Hassan Rugwa pamoja Wakuu wa Taasisi DAWASA TANROAD TANESCO na TARURA
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa