-Awataka kuzingatia mila na desturi za kitanzania wanapofanya shughuli zao
-Mkurugenzi Mtendaji Wavuvi Camp aomba radhi kufuatia clip iliyosambaa ambayo ni kinyume na maadili ya Kitanzania
- Aagiza waliojenga majengo ya kudumu COCOBEACH kubomolewa
-Apongeza Usalama ulioko, awahakikishia wananchi Ulinzi na Usalama katika Sikuu za mwaka mpya 2023
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Amos Makalla leo ametembelea na kukutana na wafanyabishara wanaofanya biashara katika fukwe za Cocobeach, Kinondoni Dar es Salaam.
RC Makalla amesema amekuja kujionea shughuli za kibiashara zinazoendelea kufanyika katika fukwe hizo na kusisitiza Coco beach ni ya Umma na itaendelea kuwa hivyo wananchi wa maeneo mbalimbali ya Mkoa huu wawe huru kutumia fukwe hii.
Aidha RC Makalla amekemea kitendo kilichofanywa na Wavuvi Camp kurekodi clip ya utupu ambayo imekua ikisambaa katika mitandao ya kijamii kinyume na maadili ya Kitanzania ambapo ametoa onyo kali na kuwataka kuwaomba msamaa watanzania.
RC Makalla ameelekeza wafanyabishara wote katika Mkoa huo kufanya biashara kwa kuzingatia mila na desturi za kitanzania.
Hata hivyo Mkurugenzi Mtendaji Wavuvi Camp Bwana Carlos Bastos ameomba radhi hadharani kwa wakazi wa DSM na Watanzania wote kuwa kilichotokea sio kusudio lao na hakitatokea tena watafanya Kazi zao kwa kuzingatia utu, maadili, mila na desturi za kitanzania
Vilevile Mhe Makalla amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Godwin Godwe pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama kutoa maelekezo kwa wanaojenga majengo ya kudumu katika fukwe, ikiwemo kubomoa jengo ya kudumu lilojengwa katika fukwe hiyo
Pia amepongeza Usalama ulioko katika fukwe hiyo na amewahakikishia Wana DSM Ulinzi na Usalama katika Sherehe za Mwaka mpya 2023
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa