-Asema mafunzo kwa viongozi kitaifa ni muhimu
-Akubali Mkutano wa Machinga Taifa Kufanyika DSM
-Uongozi wa Machinga Taifa wampongeza RC Makalla kwa ushirikiano na machinga DSM, na kuwapeleka ziara ya mafunzo Viongozi wa Machinga na Bodaboda nchini Rwanda
- Wasema Mkoa wa Dar es Salaam ni tulivu
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam CPA Amos Makalla leo Februari 14, 2023 amekubali ombi la kuwapeleka Viongozi wa Machinga Taifa nchini Rwanda ziara ya mafunzo, kufuatia Viongozi hao wa kitaifa kuwasilisha ombi hilo wakati alipokutana nao walipokuja kumshukuru na kumpongeza kwa ushirikiano wake na Machinga wa DSM katika Ukumbi wa DMDP Ilala Jijini Dar es Salaam
CPA Makalla amesema ziara za mafunzo kwa viongozi wa Kitaifa ni muhimu kwa sababu Viongozi hao wakiwa na maarifa na uelewa itasaidi kuchagiza mipango mbalimbali katika Mikoa ikiwemo ya usafi na kuwapanga vizuri wamachinga hususani DSM
Aidha CPA Makalla amekubali ombi la Mkutano wa Machinga Taifa Kufanyika DSM ombi ambalo pia liliwasilishwa kwake huku akisema Mkoa wa DSM ndio wenye machinga wengi hivyo hana pingamizi lolote juu ya Mkutano huo.
Vilevile Viongozi wa Machinga Taifa wamemshukuru CPA Makalla kwa ushirikiano wake na Machinga wa DSM kuwa nao karibu, dhamira yake ya kubadili maisha ya makundi hayo pia wamempongeza kwa kuwapeleka ziara ya mafunzo Viongozi wa Machinga na Bodaboda nchini Rwanda.
Sambamba na hilo Viongozi hao wamevutiwa na Mkoa wa DSM ulivyo tulivu wakitoa rai Mikoa mingine ya Tanzania kujifunza Dar es Salaam chini ya Uongozi wa Comred CPA Amos Makalla " wamesema Mkoa wa DSM sasa ni tulivu ndio maana wameleta ombi la kufanya Mkutano wa Machinga Taifa DSM"
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa