- Asema hajaridhizishwa na kasi ya Ujenzi atapeleka taarifa kwa Waziri mwenye dhamana
- Awahakikishia wakazi wa Makongo Juu kuwa yuko pamoja nao
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Amos Makalla amekagua maendeleo ya Ujenzi wa Barabara ya Ardhi, Makongo Juu Goba na kuonyesha kukerwa na namna mkandarasi anavyosuasua kukamilisha Ujenzi wa Barabara hiyo.
RC Makalla baada ya kukagua Barabara hiyo alipata wasaa wa kuongea na Wananchi ambao ni wanufaika wa mradi huo ambapo waliweza kumueleza kero zao zikiwemo, kuwepo kwa vifusi vya mchanga, Vumbi, kukosekana kwa mifereji ya maji, na fidia kwa kaya zilizobomolewa
Vilevile viongozi wa chama waliopewa nafasi ya kuzungumza mbele ya wananchi wameonyesha kutoridhishwa na mkandarasi anayetekeleza mradi huo wakimuomba Mkuu wa Mkoa kuingilia Kati.
Aidha RC Makalla amesema yeye binafsi ni Mara yake ya pili kutembelea mradi huo ambapo alipofika kwa mara ya kwanza na sasa haoni tofauti, hali inayomfanya kuamini mkandarasi huyo hana uwezo.
Hivyo kutokana na kusuasua uko anaenda kumpa taarifa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof Makame Mbarawa aje aitembelee Barabara hiyo na kutoa uamuzi kwa maslahi mapana ya Wananchi.
Sambamba na hilo Mhe Makalla amezipokea Changamoto zilizotolewa na wananchi na kuwahakikishia yuko upande wao yale yote ambayo yako ndani ya uwezo wake yatafanyiwa kazi kwa haraka.
Kwa Upande wa mhandisi wa Tanroad *Mwanaisha Rajabu amekiri mkandarasi wa mradi huo kuwa na kasi ndogo licha ya wao kama Tanroad kumueleza mara kea mara kuongeza kasi ya Utekelezaji wa Miradi.
RC Makalla ametoa RAI kwa wakandarasi wazawa kufanya kazi zenye ubora na kuzingatia muda ili Serikali isione sababu ya kutumia wakandarasi wa Nje
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa