- Asema ni chanzo Cha magonjwa ya mlipuko hususani Kipindupindu msimu huu wa mvua.
- Machinga wamshukuru Rais Dkt. Samia kwa kuboresha machinga complex
- Asema ujenzi soko la Kariakoo ukikamilika kipaombele ni kwa wale waliokuwepo.
- Ahamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kampeni ya Usafi.
- Awataka viongozi Na watendaji kuwa Mfano wa ushiriki wa usafi
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam CPA, Amos Makalla amepiga marufuku utaratibu wa wafanyabiashara kuuza bidhaa kwa kuzipanga chini hususani bidhaa za chakula kwakuwa ni hatari kiafya hasa msimu huu wa mvua ambapo kunaweza kutokea magonjwa ya mlipuko ikiwemo Kipindupindu.
RC Makalla ametoa onyo Hilo wakati wa zoezi la usafi wa pamoja soko la Machinga complex ambapo amewaelekeza Viongozi wa masoko yote kudhibiti na kusimamia agizo Hilo.
Aidha RC Makalla ametumia zoezi Hilo kuwahakikishia wafanyabiashara waliokuwa soko la kariakoo kuwa ujenzi ukikamilika kipaombele kitakuwa kwa wale waliokuwepo awali.
Pamoja na hayo RC Makalla ameendelea kupiga marufuku ufanyaji biashara kwenye Maeneo yaliyokatazwa na kuwataka kwenda kwenye masoko rasmi Ili waweze kunufaika na fursa mbalimbali zinazotolewa na Serikali hususani mikopo.
CPA Makalla pia ameelekeza Kila mtendaji kwenye eneo lake kuhakikisha anasimamia zoezi la usafi na kubainisha kuwa watakaoonekana kulegalega watachukuliwa hatua
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa