- Akuta Ujenzi ukiwa katika hatua za chini tofauti na Wilaya zingine ambapo Wapo hatua za mwisho
-Ashangazwa na majibu ya kuchelewa Vifaa, Ahoji kwani Wilaya zingine wameyatoa wapi?
- Awataka Madiwani kuwasimamia wananchi wake kupata vituo vya Afya
-Aagiza kufanya kazi usiku na mchana ili kumaliza kazi kwa wakati
- Awataka kwenda kujifunza kwa Wilaya ya Ubungo, Kigamboni na Kinondoni
-Mkurugenzi wa Jiji akiri kupokea maagizo yote na kuyafanyia kazi
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makalla leo tarehe 12 ameendelea na ziara yake ya kukagua Miradi ya Maendeleo katika Mkoa wa Dar es Salaam ambapo leo yupo Ilala
Akiwa Ilala ambapo ametembelea Kituo Cha Afya Cha Segerea na Kipunguni "B" Mkuu wa Mkoa ameonyesha kukasirishwa na kusuasua kwa Ujenzi wa Vituo hivyo vya Afya vya Segerea na Kipunguni "B" vilivyotokana na Fedha za Toza za Simu Shilingi Bilioni 2.5 alizozielekeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania *Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa Mkoa wa Dar es Salaam ili kutekeleza Ujenzi wa Vituo hivyo
RC Makalla ashangazwa na majibu ya Uchelewaji wa Vifaa kutoka kiwandani ndipo akahoji viwanda gani vilivyowachelewesha wao tu lakini Wilaya zingine wakapewa kwa wakati? Na Kama ilikuwa hivyo mbona hawakutafuta msaada zaidi?.
Hata hivyo Mkuu wa Mkoa amewataka Madiwani husika kuwasimamia wananchi wao ipasavyo kwa kuhakikisha wanapata Vituo vya Afya kwa wakati
RC Makalla amewaagiza Ilala kufanya kazi usiku na mchana ili kumaliza kazi kwa wakati na ubora hitajika
Vilevile Mkuu wa Mkoa amewataka baada ya kumaliza ziara yake Ilala waende wakajifunze kwa Wilaya za Kinondoni, Ubungo, na Kigamboni ili wakachukue uzoefu kwa wenzao
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Bw. Jumanne Shauri akiri kupokea maagizo yote aliyopewa na kusema atayafanyia kazi
#KAZI IENDELEE#
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa