- Asema amejiridhisha majengo hayo bado hayajapangishwa.
- Aridhishwa na namna majengo yalivyojengwa yana kidhi mahitaji yote
- Afafanua kuwa kaya 644 ndizo zitapewa.
- Awaonya matapeli wanaowalaghai Wananchi kupangisha Kota hizo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Amos Makalla leo Septemba 8,2021 amezuru na kukagua maradi wa ujenzi wa nyumba inayotekelezwa na TBA maarufu kwa Jina la *Magomeni Kota* Kinondoni Dar es Salaam.
Mradi huo kwa sasa uko katika hatua za mwisho kukamilika kinachomaliziwa ni mifumo ya Umeme katika eneo hilo kuna majengo ya gorofa 5 bustani na sehemu nzuri za michezo.
Mhe Makalla amesema amekuwa akipata taarifa nyingi wengine wanasema majengo tayari yameshapangishwa na wengine wakimuomba awasaidie kupata nyumba hizi, hivyo ujio wake ni kujiridhisha.
Mkuu wa Mkoa amejiridhisha kuwa hakuna aliyepangishwa, ameendelea kumpongeza Rais wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan kwa dhamira yake ya kuendelea kutekeleza miradi iliyoachwa na mtangulizi wake, Magomeni Kota ni moja kati ya miradi mingi inayotekelezwa hapa nchini.
Amebainisha kuwa wakazi waliokuepo katika eneo hilo wapatao kaya 644 ndio watakaopewa nyumba hizo na wataishi miaka 5 bila kulipa pango kama maelekezo ya awali yalivyokuwa.
Aidha ametoa onyo kwa matapeli kuacha kuwalaghai watu kuwa kuna nafasi ya kupanga katika majengo hayo.
Vilevile Mhe Amos Makala amewataka TBA kuwa na maono ya mbali au kuwa na mpango mkakati wa matumizi bora ya Ardhi katika eneo lililobaki kwani Dar es Salaam kwa sasa Ardhi haitoshi.
Ifahamike kuwa mradi wa Magomeni Kota ulianzishwa na aliyekuwa Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt John Pombe Magufuli na maagizo yake yalikuwa mradi ukikamilika kaya 644 ndio watapewa kipaumbele katika majengo hayo na wataishi kwa muda wa miaka 5 bure bila kulipa kodi.
ReplyForward |
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa