- Amshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa msukumo wake kuridhia kutoa fedha kukamilisha miradi hiyo ya maji
- Atangaza Disemba 15 maji yataanza kupatikana rasmi katika maeneo hayo
-Awataka wakazi wa maeneo hayo kuchangamkia fursa ya kuunganishwa maji
-Aagiza DAWASA kuhamasisha wananchi kuunganishiwa maji na kuzingatia muda alioutoa kwa wakazi kupatiwa maji
- DAWASA watoa offer kwa wateja wa maji kukopeshwa malipo badae Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Amos Makalla leo ametembelea na kukagua miradi ya maji ya zaidi ya Bilioni 75 ambayo itawanufaisha wakazi wa Goba, Tegeta, Wazo, Bunju, Mabwepande na Mapinga ambao kwa Kipindi kirefu walikua wana changamoto ya Maji.
RC Makalla amekagua Ujenzi wa matenki yenye uwezo wa kuhifadhi maji lita milioni 6 na pampu za kisasa, hivyo kuwezesha maji kuwa na "pressure" ya kutosha pale yanaposambazwa kwa wananchi.
Aidha RC Makalla amemshukuru Rais Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa msukumo wake wa kuridhia kutoa fedha ambayo imewezesha Kufanikisha kukamilika kwa miradi hiyo ya maji
Hata hivyo RC Makalla ametangaza ifikapo Disemba 15 mwaka huu maji yataanza kupatikana hivyo amewataka wananchi na wakazi wa maeneo hayo kuchangamkia fursa ya kuunganishwa maji.
Vile vile ameagiza DAWASA kuendelea kuhamasisha wananchi kupitia Idara yao ya Mawasiliano kwa Umma ili wananchi waweze kuunganishiwa maji katika kaya zao, waepukane na kadhia waliyokuwa wanaipata kwa muda mrefu
Kwa Upande wa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema Wananchi watakao hitaji kuunganishiwa maji sasa watakopeshwa malipo yatafanywa kidogo kidogo kwa Kipindi cha mwaka wanachotakiwa sasa kupeleka maombi katika Ofisi za DAWASA zilizoko karibu nao
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa