- Akagua Jengo la Utawala Kinondoni, Ujenzi wa Kituo cha Daladala na Uwanja wa Mpira Mwenge
- Asema Miradi hiyo ilisimamishwa na Waziri wa TAMISEMI amekuja kuiona na kujiridhisha
- Asema Miradi hiyo ni muhimu licha ya kuwa na Changamoto ndogo ndogo siku za usoni atatoa tamko la kuendelea kwa maandishi
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Amos Makalla leo Oktoba 29, 2021 amekagua miradi 3 ya maendeleo ambayo ni Ujenzi wa Jengo la Utawala Manispaa ya Kinondoni, Ujenzi wa Uwanja wa Mpira na Kituo cha Daladala Mwenge - Kinondoni, Dar es Salaam.
Mhe Makalla akiwa katika Jengo la Utawala Manispaa ya Kinondoni amesema lengo la ziara yake ni kukagua miradi hiyo na kujiridhisha na baadaye atatoa tamko kwa maandishi ili miradi hiyo iweze kuendelea huku akibainisha tamko lake litaelekeza kuziondoa Changamoto ambazo zilikuwepo zilizopelekea kusimama kwa miradi hiyo.
Mkuu wa Mkoa amebainisha Miradi hiyo ilisimamishwa na Waziri wa TAMISEMI Mhe Ummy Mwalimu baada ya kuonekana ina Changamoto, akatoa maelekezo ya kuchunguza dosari hizo kupitia tume ambayo iliundwa chini ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, uchunguzi umeshafanyika siku si nyingi atatoa Tamko kwa maandishi la kuendelea kwa miradi hiyo
Aidha Mhe Makalla akiwa Mwenge kituo cha Daladala na Uwanja wa Mpira amesema miradi hiyo ni muhimu ikikamilika itaongeza mapato ni vema ukamilishwaji wake uwe na mtazamo wa Kibiashara kwa mfano uwanja wa mpira uwe na eneo la "parking" pia taa za umeme ili uweze kutumika usiku na mchana.
Amesisitiza anatarajia kuona miradi hiyo inakamililishwa kwa kuzingatia ubora na thamani ya pesa "Value for Money"
Aidha Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Godwin Gondwe amesema amepokea maelekezo ya Mkuu wa Mkoa tayari kwa Utekelezaji kwa maslahi mapana ya wananchi na Taifa
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa