-Awataka Kujikwamua kiuchumi, Kurejesha mikopo kwa wakati
- Ameelekeza Manispaa zote tano DSM kutoa mafunzo kwa wanufaika wa mikopo ya 10%
- Amezitaka Mamlaka za udhibiti ubora bidhaa kutoa huduma rafiki kwa wajasiriamali wadogo na Mabenki kutoa elimu ya fursa zilizoko
- Amshukuru Rais Dkt Samia kwa kuelekeza Mamlaka za mitaa nchini kutenga fedha za mikopo bila riba kutoka katika mapato yake ya ndani
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam CPA Amos Makalla leo Machi 20,2023 amekabidhi hundi ya Bilioni 4.6 ya mikopo ya asilimia 10 kwa vikundi 185 vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu Manispaa ya Temeke katika viwanja vya Shule ya Sekondari Kibasila Jijini Dar es Salaam
CPA Amos Makalla akikabidhi hundi hiyo amewataka wanufaika wa mikopo hiyo kutimiza kusudio la utoaji wa mikopo kuhakikisha wanajikwamua kiuchumi na Kurejesha kwa wakati ili kutoa fursa kwa wangine kupatiwa mikopo hiyo.
Aidha CPA Makalla ameelekeza Manispaa zote za DSM kutoa mafunzo kwa wanufaika wa mikopo hiyo ili pesa wanazokopa ziweze kutumika kwa kuzingatia kusudio la ombi la mkopo wazalishe bidhaa wapate masoko na kujiongezea kipato.
Hata hivyo CPA Makalla amezitaka mamlaka za udhibiti ubora wa bidhaa kutoa huduma rafiki kwa wajasiriamali pasipo kuwakatisha tamaa,pia Taasisi za kifedha ziendelee kutoa elimu na fursa zilizoko katika taasisi hizo kwa wajasiriamali
CPA Amos Makalla vilevile amemshukuru Rais Dkt Samia kwa kuelekeza Mamlaka za mitaa kote nchini kutenga asilimia 10 ya mapato yake kwa ajili ya mikopo ya makundi maalum ambao ni 4%Wanawake,4%Vijana na 2%Watu wenye Ulemavu
Mwisho CPA Makalla ameipongeza Manispaa ya Temeke kwa kitenga kiasi hicho kikubwa cha pesa pamoja na Pikipiki na bajaji kuwakopesha makundi maalum, ni takwa la kikatiba na wengine waige mfano huu
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa