- Apiga marufuku tabia ya abiria kutupa taka nje hovyo
- Asema Kampeni ya SAFISHA PENDEZESHA DAR ES SALAAM ni endelevu.
- Ashukuru Kampuni ya Wese kwa kushirikiana na Serikali ya Mkoa.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amegawa Vibebea taka (dustbin) 1,000 kwa Daladala 1,000 zinazofanya safari maeneo mbalimbali ya mkoa huo ambapo amepiga marufuku tabia ya abiria kutupa taka hovyo.
Akikabidhi Vifaa hivyo vilivyotolewa na Kampuni ya Wese Tikisa Tanki, Piga Bao, RC Makalla amesema Serikali kwa kushirikiana na Wadau wamefanikiwa kugawa Vifaa vya kuhifadhi taka kwenye maeneo mbalimbali ya mkoa huo ili kuhakikisha Wananchi wanapata sehemu za kutupa taka.
Aidha RC Makalla ameelekeza Madereva na Utingo kuzitumia dustbin hizo kwa lengo lililokusudiwa ikiwa ni pamoja na kuwakemea abiria watakaojaribu kutupa taka nje.
Pamoja na hayo RC Makalla amepongeza Kampuni ya Wese kwa kushirikiana na Serikali ya Mkoa huo kwenye suala la Usafi na kutoa wito kwa Wadau wengine kujitokeza.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa