Baadhi ya viongozi na wananchi wa makundi mbalimbali wakiwa katika hafla ya IFTAR katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam jioni ya leo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam CPA, Amos Makalla leo April 14 amefuturisha Mamia ya Wananchi wa Mkoa huo katika Futari iliyohusisha viongozi na wawakilishi wa makundi mbalimbali Katika jamii.
Akizungumzia wakati wa Hafla hiyo iliyofanyika Viwanja vya Karimjee, RC Makalla ametoa wito kwa Wananchi kuendelea kudumusha umoja wa kidini uliopo baina ya wakristo na Waislamu.
Aidha RC Makalla ametumia hafla hiyo kumtangaza Sheikh Walid Alhad Kawambwa ambae ni Kaimu Sheikh wa Mkoa huo kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Amani ya Mkoa huo na kutoa wito kwa Wananchi kumpatia ushirikiano Ili kuendelea kudumusha amani.
Kwa Upande wao baadhi ya Wananchi waliopata fursa ya kushiriki hafla hiyo wamemshukuru RC Makalla kwa mwalio na heshima kubwa aliowapatia na wameahidi kuendelea kushirikiana nae katika masuala mbalimbali.
Futari ya Mkuu wa Mkoa imehusisha Wananchi wa makundi yote wakiwemo *Viongozi wa kiserikali, viongozi wa Dini zote, Viongozi wa Taasisi, Machinga, Bodaboda, Yatima, Wajane, Wenye ulemavu na wasiojiweza na wadau wengine.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke kulia Mhe Mwanahamis Munkunda akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe Halima Bulembo kushoto wakati wa hafla ya IFTAR iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa CPA Amos Makalla.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa