-Ampongeza Rais Dkt Samia kwa kuwezesha Sensa Kufanyika kitaalam, Kisasa, na kuratibiwa vizuri
- Asema huwezi kuwa na mipango ya maendeleo bila kuwa na takwimu sahihi
-Abainisha hata watafiti, wachumi, hutegemea takwimu sahihi, na sasa Taifa lina takwimu sahihi kupitia sensa ya mwaka 2022
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam CPA Amos Makalla leo Machi 24, 2023 amefungua semina ya Usambazaji na Uhamasishaji wa matumizi ya matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 kwa Madiwani, Watendaji wa Kata, Mitaa na Wenyeviti wa Mitaa wa Mkoa wa Dar es Salaam, Semina ambayo imefanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee.
Akifungua Semina hiyo CPA Amos Makalla amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuweka historia ya kuwezesha Sensa Kufanyika kitaalam Kisasa na kuratibiwa vizuri nchi nzima kaanzia maandalizi, wakati wa Kuhesabu hadi kutoa matokeo ya Sensa
Aidha CPA Makalla amesema huwezi kupanga mipango ya maendeleo katika nyanja yoyote ile bila kuwa na takwimu sahihi, Tafiti zozote zinazofanyika zinahitaji takwimu sahihi hata kujua pato la mtu mmoja mmoja nchini lazima uwe na takwimu sahihi.
CPA Makalla ameipongeza Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa kusimamia vema zoezi la Sensa ya Watu na Makazi na kuandaa Semina ya Usambazaji na Uhamasishaji wa matumizi ya matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi kwa Viongozi hao ambao wapo karibu na Wananchi katika ngazi ya chini kabisa kwenye mitaa
Mwisho CPA Makalla ametumia fursa hiyo adhimu kuutangazia Umma kuhusu Ujio wa Makamu wa Rais wa Marekani Mhe Kamala Harris Machi 29, 2023 Tanzania na atafanya Ziara Jijini Dar es Salaam
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa